Ungeweza kuwasiliana nao kwa kupitia hiyohiyo App yako inayozingua lakini,
Ili mambo yasiwe mengi fanya yafuatayo:
-Ingia kwenye Website yao (
WhatsApp) na shuka chini kabisa,
Tafuta/Ingia
Technical Support,
Itakupeleka sehemu ya kuchagua unataka msaada eneo gani,
Chagua
WhatsApp Messenger Support,(Mara nyingi inakuwa ndio ya kwanza kwenye hiyo List)
Utaletewa Form ya kujaza taarifa kadhaa ikiwemo Email address, aina ya kifaa unachotumia kuingia WhatsApp,
Namba ya simu yako ambayo umeitumia kujisajili WhatsApp vilevile kuna
Ki-Box ambapo wanataka uweke ujumbe (
Message) Maana yake hapo useme unahitaji msaada wa aina gani/Uelezee shida yako kwa kifupi.
Hapa usijifanye mzungu sana,
Andika tu kuwa (Wamekufungia na wamefanya hivyo
KIMAKOSA)
Na hivyo basi unawaomba wakufungulie
(Kwa Lugha ya-Kiinglish) lakini.
Baada ya hapo bonyeza
NEXT.
Muda sio mrefu watakutumia ujumbe na-pengine kukufunguli moja wa moja.
KUMBUKA, Hii ni iwapo ni kweli huna
makandokando kwenye Matumizi yako.
Kama umeripotiwa wewe kutumia App ndivyosivyo jua inaweza kuwa changamoto.
Nawasilisha.