Naomba msaada wa ajira yoyote. Nina shida ya usikivu hafifu

Naomba msaada wa ajira yoyote. Nina shida ya usikivu hafifu

Uchepe

Member
Joined
Feb 5, 2024
Posts
5
Reaction score
12
Habari za Uzima Ndugu zangu.

Mimi ni Kijana wa Kiume Mwenye Umri wa Miaka 26 Nina Usikivu Hafifu. Hali hii imenifanya Nakosa Kazi / Mishe.

Juzi Niliitwa kwenye Usaili Kwenye Kampuni Ya Ulinzi Ya
"Ws insight Security" iliyopo Msasani. Usaili Nilifanya Vizuri Lakini walipogundua Nina Usikivu Hafifu Wakanikataa. Kiukweli Niliumia sana, Maana Nilitegemea Hiyo kazi niweze Kupata Mtaji wa Biashara.

Kwenye Kampuni Nyingine ya insight iliyopo Mwembe Yanga Boss Wao pia Akanikataa. Daah.

Ndugu zangu kwa kifupi Mimi Nimesoma Mpaka kidato Cha Sita.

Ada ilikosekana ya Chuo hivyo nikaingia Mtaani Kupambana.

Nimehangaika Sana Huku na huku Bila Mafanikio.

Wahenga walipata kusema "Mficha Uchi Hazai" hivyo
Ndugu zangu Naombeni Mnisaidie.

Kazi Yoyote ya Halali Nitafanya.

Nipo Chini ya Miguu Yenu Ndugu zangu. Naombeni Mnisaidie Mimi Mdogo Wenu.

Naishi Temeke, Dar es Salaam.
 
Mungu akusikie na akupe hitaji la moyo wako
 
Kila la kheri ndugu yangu, kazi ya ulinzi ukiwa na usikivu hafifu siyo nzuri kiusalama nakuombea upate kazi nyingine bora zaidi.
 
Pole kiongozi, unge edit hapo ulipoandika ulikua unatafuta kazi upate mtaji uanzishe biashara yako, kuna mtu anaweza akawa anataka mtu wa muda mrefu akaona Hio akakuacha maana inakera sana unam train mfanyakazi muda mrefu anakuja ghafla kuacha unaanza tena kutafuta mtu mpya
 
Pole kijana. Utapata.

Ila usiwe unaandika vitu visivyo vya kweli next time. Internet haisahau.

Hope umenielewa.

Unamaanisha huu uzi aliotuambia ana 28?na ana elimu ya chuo?

Unamaanisha huu uzi aliotuambia ana 28?na ana elimu ya chuo?

acheni kumsagia kunguni
 
hao jamaa walikukataa walikuwa sahihi kazi ya ulinzi na ww unamatatzo ya kusikia hiyo ni hatari kwako ww mwenyewe,
 
Pole sana mkuu nina tatizo la usikivu hafifu kama wewe kwenye suala la kupata kazi kuna changamoto sana. Mimi mpaka vyeti vya chuo nishafungia kabatini nimekubali nilikosea kukomaa na kitabu kwaiyo nimeanza upya, bado mambo yangu hayajakaa sawa ila nasikitika sana muda niliopoteza chuo bora ningesomea ufundi. Endelea kupambana mdogo angu haupo peke yako.
 
Back
Top Bottom