Naomba msaada wa haraka sana mdogo wangu anaharisha.

Linamo

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2011
Posts
9,976
Reaction score
24,496
Habari jf.
Nina mdogo wangu toka jana anaharisha maji maji yenye makamasi yenye rangi ya kahawia ametumia erthromine (sijui kama nimeiandika sawa) bila mafanikio Leo akatumia dawa iliyoandikwa norzole kwa ajili ya kuzuia kuharisha lakini bado anaharisha.
Naomba ushauri atumie nini ili akate kuharisha.
Natanguliza shukrani.
 
Pole sana, naona hapo ndugu hembu muwahishe hospitali ili wajue ni nini, ndio watampa dawa sahihi. Ila kwa jinsi ulivyoeleza kuna uwezekano mkubwa akawa na amoeba na kuna dawa nzuri sana kwa ajili ya ugonjwa huo, ila apate kwanza vipimo.
 

Wewe ni daktari au huyo mgonjwa ni daktari? Maana naona dawa zote mnazijua!
 

Wahi hospitali haraka acha mambo ya JF hapa!
 

Pole sana, naona hapo ndugu hembu muwahishe hospitali ili wajue ni nini, ndio watampa dawa sahihi. Ila kwa jinsi ulivyoeleza kuna uwezekano mkubwa akawa na amoeba na kuna dawa nzuri sana kwa ajili ya ugonjwa huo, ila apate kwanza vipimo.

Hiyo norzole tabs ni dawa nzuri sana ina mchanganyiko wa tinidazole na norfloxiacilin na hainyweki chini ya umri wa miaka 15 ila ni vizuri sana tuwe na utamaduni wakupima ili ujue chanzo na unachokitibu ni nini kwa wakati husika zaidi ya hapo kupenda kunywa dawa bila ushauri wa daktari ni kulazimisha figo kuchuja sumu zaidi ya uwezo wake na ndio maana maradhi ya figo yanaongezeka kila uchwao.
 
Humu unapoteza muda...kimbia hosp baada ya hapo ndo uje huku...huku wengine washereheshaji tu
 
mpige gunzi huko chini,tatizo likizidi mwone Dr
 
Chukua majani mateke ya mpera yatwange vzur alaf changanya na maji ukumbuke kuchuja kisha mpe kwenye kikombe kdgo cha chai anywe mara 1 alaf ckilizia.
 
mpe asali kidogo ili apunguze kuharisha then mpeleke hospital
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…