Naomba Msaada wa Kibarua

Naomba Msaada wa Kibarua

Joined
Apr 12, 2023
Posts
10
Reaction score
14
Hodi na Salamu Members.

Mimi ni kijana wa kiume (27), Elimu yangu ni ya Secondary.

Nimekuja kwenu Kuomba Connection ya Kibarua cha kulipwa kwa siku, Nimeandamwa na msururu wa Madeni ya Kodi na kwa mangi.

Nipo tayari kufanya Majukumu yoyote ilimradi yasikiuke Utu na sheria za nchi.
Mungu amuinue mtu kwajili yangu, Amen

Naishi Dar es salaam.
 
Habari ya Usiku Ndugu yangu wa JF.

Mimi ni kijana (me) nna Mke na mtoto Mmoja, naishi Dar es salaam. Ndugu yako/yenu nimeandamwa na Majukumu ya Kodi na pesa ya kulisha familia.

Shime naomba kwa yeyote mwenye kuguswa anisaidie Kibarua Ili nipate kuondokana na Msongo wa Majukumu.

La Kuna MTU anayejua viwanda vitoavyo KAZI kwa vibarua au Kuna sehemu ya saidia fundi kujenga ama KAZI yoyote halali aniunganishe Tafadhali. Nitadhalilika Ndugu yenu.

Nna elimu ya Sekondari pekee, najua hesabu zote na Niko vizuri kwenye matumizi ya Kompyuta.

Mungu akubariki utakayesoma jumbe hii

Asante
 
Sehemu za vibaru.
Masokoni mfn mabibo sokoni.
Site hamnaga kuomba ruhusa bali kuomba kazi. Nenda utapewa.
Ungekua na kamtaji ningekwambia kimbiza udalali wa nyumba, magari, na vitu vyvyte.
La mwisho.
Usiogope kufanya chchte kwa hali ulionayo. Msongo wa mawazo ukizidi utalala sana ndani. Amka kapige kazi ndugu.
 
Habari za pilika ndugu zangu.

Nimerudi tena Ndugu zangu, bado sijapata kazi tangu niombe msaada humu ndani.

Leo naomba Mnisaidie walau majina ya viwanda vitoavyo kazi kwa hapa Dar es salaam Ili niweze kujaribu bahati yangu.

Hali ni mbaya Wakuu, nimebanwa na madeni kila kona.

Naombeni msaada
 
Akili nyingine nenda stand ya daladala karibu yako, ulizia dei waka ya ukonda wa daladala, makonda wengi wanachoka hvo huwa wanapokezana kuamka saa 10 kulala saa nne sio kaz ndogo, hukosi kaz ya ukonda wa daladala uwe mwaminifu na ujue vituo vya route unayoomba kaz
 
Au nenda kurasini kuna yard kibao za magari, omba kazi ya kuosha magari, jenga mazoea na madereva, tengeneza uaminifu jipendekeze anza na utingo, jifunze gari ukiaminika tafuta chet na leseni anza kaz ya udereva rasmi, maisha ni safar mguu wa kutoka una baraka zake
 
Au nenda mjini pale posta kuna parking kubwa ya magari, inaangaliana na wizara ya mambo ya ndani, waone jamaa pale waambie mi muosha magari jitambulishe vzuri, ukielewana nao wahi mapema siku inayofuata anza kazi. Kuosha gari moja 3,000 zinapaki gari zaid ya 50 huwez kosa gari 5 mpaka 10 za kuosha kila siku. Walionza pale saiv wengi wameajiriwa na posta kukusanya mapato sijaona muosha magari mpya hivi karibuni wahi mapema pale
 
Habari za pilika ndugu zangu.

Nimerudi tena Ndugu zangu, bado sijapata kazi tangu niombe msaada humu ndani.

Leo naomba Mnisaidie walau majina ya viwanda vitoavyo kazi kwa hapa Dar es salaam Ili niweze kujaribu bahati yangu.

Hali ni mbaya Wakuu, nimebanwa na madeni kila kona.

Naombeni msaada
unatafuta kazi ya aina gani maeneo gani maana isije ukawa kama kijana mmoja alinishangaza amehitimu SUA masuala ya kilimo lakini hataki kazi za susimaimizi shambani anataka mwanzoni tu akiajiriwa apate kazi ya ofisini kwenye kiyoyozi.
 
unatafuta kazi ya aina gani maeneo gani maana isije ukawa kama kijana mmoja alinishangaza amehitimu SUA masuala ya kilimo lakini hataki kazi za susimaimizi shambani anataka mwanzoni tu akiajiriwa apate kazi ya ofisini kwenye kiyoyozi.
Nipo dar es salaam.
KAZI yoyote halali Mkuu

Elimu yangu ni ya Sekondari
 
Back
Top Bottom