Naomba msaada wa kidaktari

Naomba msaada wa kidaktari

Ba Chomsky

Member
Joined
Feb 18, 2013
Posts
20
Reaction score
2
Ndg zangu habari za majukumu. Mwanangu anauvimbe sehemu ya chini ya mbavu kushoto kuelekea kwenye tumbo.Uvimbe huo ni kama mfupa lakini sio. Wenye kujua hili tatizo karibuni kwa msaada. Mtoto anaumri wa mwaka 1 na miezi 3. Karibuni.
 
Uvimbe uko kwa ndani (yaani ndani ya tumbo) au kwa nje (kwenye ngozi au misuli ta ukuta wa tumbo)?

Mtoto huwa anapata matatizo ya kupungukiwa na damu, manjano ya macho, homa za mara kwa mara?...ni vigumu kusema kwa uhakika maana umetaja dalili moja tu, lakini inaweza kuwa uvimbe wa 'bandama' (Spleen). Mpeleke mtoto hospitali akachunguzwe.

Uvimbe wa bandama mara nyingine yaweza kuwa ni tatizo kubwa hasa kwenye mfumo wa damu.
 
Ndg zangu habari za majukumu. Mwanangu anauvimbe sehemu ya chini ya mbavu kushoto kuelekea kwenye tumbo.Uvimbe huo ni kama mfupa lakini sio. Wenye kujua hili tatizo karibuni kwa msaada. Mtoto anaumri wa mwaka 1 na miezi 3. Karibuni.

Mkuu kwanini huo mida unaotumia ku post humu usiende hospital?? Kwani mambo ya afya sio kama computer/simu unaleta humu kuwa computer yangu ina mawenge haya, wataalamu wanakuja na kukupa soln, lakini sio kwenye afya tena ya mtoto!!

Mpeleke kwenye vipimo mkuu, kuna jamaa aliomba humu ushauri wa ki daktari akatokea mwehu mmoja aka pm, kumbe dawa yenyewe ni viagra tena alimuuzia mwenyewe habari yake aliipata, hadi leo alisababisha tatizo lingine. Kwani humu ma bush dr.

Ni wengi sana mtu alisoma zile chemical equestions, za form 2,na biology kidogo anajiita le dokteriii!!!vitu vya electronic hata ukiingia chaka mwenyewe, litaungua tu, lakini sio mwili wa binadamu mkuu.
 
Ahsante ndg.uvimbe uko kwa ndani. Yaani ukimgusa unahisi kama mfupa fulani hivi ambao ni kama ubavu, akilalia mgongo unatokeza,ilhali upande wa pili hali kama hii haipo. Ila wacha nimpeleke hospital for more check up.
 
Back
Top Bottom