Naomba msaada wa kisheria kukomesha uhuni wa Halotel

Naomba msaada wa kisheria kukomesha uhuni wa Halotel

Capital

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2010
Posts
1,468
Reaction score
1,063
Wakuu,

Niende kwenye hoja moja kwa moja.

Wiki mbili zilizopita nilikosea kutoa muamala wa pesa kwa wakala wa halopesa kutoka kwenye line yangu ya halotel na dakika hiyo hiyo nikawapigia huduma kwa wateja na wakaisimamisha na kisha wakanitumia namba ya uthibitisho.

Na maelezo niliyopewa ni kuwa pesa yangu ingerejeshwa kwenye acct yangu kati ya saa 24 -72.

Tokea masaa 72 yalipoisha, sijawahiona kitu. Kila nikiwapigia simu wananipa majibu ya janja janja. Nimepoteza mengi kutokana na halopesa kutonilipa pesa zangu halali.

Ombi langu naomba kama kuna wanasheria wenye uwezo mkuje mnisaidie nione hawa wahuni wana nini wanachoringia wakati pesa ni zangu.

Asanteni
 
Halotel ni wapuuzi, niliunga gb 1 nikaweka sim card kwenye router yao naku connect kwenye pc (updates zilikuwa off) huku nikitumia JF mb zikaisha ndani ya nusu saa, nikaunga tena kwa kutumia kwenye simu nayo ikaisha haraka
kuwapigia, muhudumu namuuliza anatoa majibu hayaeleweki ananiambia nimezitumia, nikamuuliza zimeishaje haraka hivo hana majibu
 
Halotel ni wapuuzi,niliunga gb 1 nikaweka sim card kwenye router yao naku connect kwenye pc (updates zilikuwa off) huku nikitumia JF mb zikaisha ndani ya nusu saa,nikaunga tena kwa kutumia kwenye simu nayo ikaisha haraka
kuwapigia,muhudumu namuuliza anatoa majibu hayaeleweki ananiambia nimezitumia,nikamuuliza zimeishaje haraka hivo hana majibu
Kwenye suala la Mb kuisha haraka halotel inaogozwa kulaumiwa hata mimi nikijiunga bando la halotel data natumia kwa wasiwasi tofauti na Kwengine na wkt mwingine bando haliishi nihalahi nikiangalia kwny data usage.
 
Kwenye suala la Mb kuisha haraka halotel inaogozwa kulaumiwa hata mimi nikijiunga bando la halotel data natumia kwa wasiwasi tofauti na Kwengine na wkt mwingine bando haliishi nihalahi nikiangalia kwny data usage.
hapa nafikiria nipeleke router mjini mafundi wafanye namna isome sim card ya Tigo
 
hapa nafikiria nipeleke router mjini mafundi wafanye namna isome sim card ya Tigo
kwaujumla mitandao yote ya simu tunayotumia hapa tanzania ni ya kiubabaishaji kifupi tu hakuna mtandao wa maana hata mmoja, yaani kila mtandao unachangamoto zake sema tofauti ni ukubwa tu wa changamoto, sisi wengine tunatumia mtandao wa tigo, cha kusikitisha tangu kampuni ilivyobinafsishwa ni matatizo mwanzo mwisho imefikia hatua mpaka tunatoleana maneno ya kashfa na customer service, yaani tigo walivyo una report changamoto hii sasa hivi haipiti hata lisaa unakumbana na vhangamoto nyingine, ipo siku mtaona tu umu jukwaan tunaichafua kampuni endapo wataendelea na ujinga wao. unaweza ukanunua kifurushi cha mwezi iwe data, text ama voice call, utatumia kwa muda wa lisaa au masaa kadhaa unakuta huduma zina fail na tayar wameshakukata pesa yako. yaani kama kuna mtu wa tigo anasoma hili bandiko basi taarifa hizi azifikishe mapama sana sababu naendelea kukusanya ushahidi muda si mrefu nitakuja kukichafua umu jukwaan
 
Watu wanakusanya Hasara za Magu. Sasa hivi ni kuwa Makini sana usiingie kwenye Kumi na Nane za Mtu mwenye Pesa hutopata Haki.
 
Halafu hivi ukisharenew line,mfano nikirenew line ya HALOTEL wanaifungua baada ya muda Gani ? YAANI inaanza kufanya kazi baada ya muda Gani ?
 
Back
Top Bottom