Pamoja na matatiza ya "spellings" katika meseji yako, nimekuelewa kuwa umerithishwa
ardhi ambayo uliyemrithi alikuwa akiimiliki kwa muda mrefu hujasema kwa muda gani
na pia aliipataje. Aidha hujasema ardhi hiyo imepimwa au inamilikiwa kimila? Pia hujafafanua madai
ya huyo anayedai kuwa ardhi hiyo ni yake, aliipataje na lini na ni vipi ilimilikiwa na huyo unayedai kuwa
alikurithisha, lazima hadithi zote mbili ziwe bayana ili upate ushauri wa kitaalamu hapa, ila mwisho wa siku
ni muhimu ukatafuta mwanasheria/wakili kwani huenda habari nyingine ukiziweka hapa zinaweza
kumnufaisha mpinzani wako, ila kama unaweza kuziweka kwa namna ambayo itatunza siri ziweke kwa kujibu
maswali hayo muhimu ili wataalamu wakuchangie mawazo.