Mimi ni mpangaji ambaye mwenye nyumba wangu hakunipa mkataba wowote wakati naingia kwenye nyumba yake, mwanzoni mwa mwezi huu wa kwanza aliniletea notisi inayoeleza kuwa mwisho wa mwezi huu inatakiwa nihame kwa sababu anataka kuhamia kwenye nyumba yake, hata hivyo kodi yangu imeisha trh 6/1/2013. tatizo ni kwamba mwenye nyumba analazimisha kuleta mafundi wa kufanya matengenezo ndani kwangu wakati mimi na vitu vyangu nikiwa bado naishi kwenye hii nyumba yake. Jamani hii ni sahihi? kama si sahihi nifanyeje?....msaada tafadhali