Mwenye nyumba anatakiwa kukupa notisi ya Siku 30 kama anahitaji uhame. Uwe na mkataba wa maandishi au la. Baada ya siku 30 unatakiwa uhame vinginevyo ana haki ya kumleta Dalali wa Mahakama kukuondoa kwa gharama zako. Kabla ya siku 30 kuisha mwenye nyumba hana haki ya kukubughudhi kwa namna yoyote ile kama kwa kuleta mafundi, kukufungia nje n.k. Akifanya hivyo una haki ya kumshitaki kwenye Baraza la Kata au Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya.