Naomba msaada wa kitabibu juu ya huu ugonjwa

Naomba msaada wa kitabibu juu ya huu ugonjwa

Ndugu yangu

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2013
Posts
676
Reaction score
359
Wana Jf habari za jumapili?

Kwanza kabisa naanza kwa kutoa pongezi kwa Jamiiforum Doctors kwa kazi nzuri za ushauri na msaada wa kitalaam mnaoutoa kwenye hili jukwaa.

Mimi nina sumbuliwa na ugonjwa ambao nashindwa kuuelewa unasababishwa na nini, nina mafua yaliyoganda ndani ya koo la hewa nikipenga huwa hayatoki hadi nizibe tundu moja la pua huku nikivuta pumzi kwa ndani, nikishavuta yanashuka juu ya taya na kuyatema.

Nina mda mrefu sasa, nilishawahi kutumia dawa za hosipitali aina ya centirizine dihydrochoride hali ikawa nzuri, lakini nilipo maliza dozi baada ya mda wa miezi kama miwili hali ilirudi tena.

Kwa anayejua tiba ya ugonjwa huu naomba msaada. Natanguliza shukrani zangu kwenu nyote. Akhsanteni
Mungu awabariki
 
ushaur fanya mazoez ya viungo hasa kukimbia mbio kwa umbal mrefu hasa wakat wa asubuh.....Inaweza kukusaidia kwa kias flan kupunguza tatzo km si kuacha kabixa..
 
hata mm nina tatizo hilo mwaka wa pili sasa natumia predinisolone kupunguza tu makali lkn nilifanya CT scan ya sinus aghakan nikaambiwa septum yangu imehama ndio maana makamasi yanakosa mwelekeo na kushuka kooni na inabidi nipasuliwe kurekebisha mpaka sasa sijafanya decision namtafutaENT mzuri cause ni surgery ipo complicated sijui ww umefikia wApi na tatizo lako
 
Back
Top Bottom