Kiparamoto
Senior Member
- Oct 1, 2015
- 100
- 100
Salaam wakuu,
Mimi ni kijana mpambanaji na mhitimu wa chuo nipo mjini Dar es salaam, katika kupambana na maisha na ukosefu wa ajira nimejitahidi kufanya biashara mbalimbali ambazo zimeweza kunifikisha hapa nilipo.
Nimefanya sana biashara ya nafaka mbalimbali na kuku kutoa mikoani kuleta huku mjini, ila kutokana na changamoto mbalimbali nilishindwa kuendelea na biashara hizo.
Katika kujichanganya mjini nilipata fursa ya soko la samaki aina ya kaa na pweza ambapo kuna jamaa alikuwa ananunua kwa bei nzuri tu then yeye huenda kuuza kwa mahotel/migahawa ya wachina (nilipewa fununu na watu). Baada ya kuzungumza nae nikatafuta mahali kwa kupata samaki hao kwa bei nzuri na kisha kuanza kupeleka kwa jamaa.
Biashara ilionyesha kulipa, lakini cha kushangaza baada ya kupeleka mzigo mara mbili jamaa akaanza kunitolea nje akisema kwa sasa hana soko (hakutaka kuzungumza kiundani zaidi) ni kama hamna tena biashara inayoendelea baina yetu tena, ukizingatia tayari nishapata uwakika wa samaki ninapoenda kuchukua.
Lengo la uzi huu ni kutaka msaada wa soko la hao samaki (Pweza, kaa, ngisi) kwa yeyote anaejua au kufahamu mahali kwenye soko la uhakika.
Natanguliza shukrani.
Wasalaam.