FUNDI H.JOHNSON
New Member
- Sep 23, 2011
- 2
- 0
Mama yangu alilalamikiwa katika baraza la ardhi na nyumba wilaya mwaka 2010, aliweza kufika mahakamani mara chache kwani alizidiwa ugonjwa na hatimaye alifariki (2014), ingawa tulikuwa tukienda kumuagia mwenyekiti mara nyingi alitukatalia na hata nilipofikisha maelezo ya kupinga rufaa ile aliyakataa akasema yanapaswa kuandikwa na mwanasheria! Hatukuwa na uwezo wa kifedha kupata huduma ya wakili! Wakati shauri hili linaendelea mahakamani mkata rufaa alikuwa akilikodisha shamba lililokuwa kwenye mgogoro nilipompa taarifa mwenyekiti alinipuuza, mwaka 2013 nilipoenda mahakamani kuulizia kuhusu shauri hili nikaambiwa limekosa mwenyewe hakuna upande unaohudhuria ingawa limefika kwenye kutoa hukumu. Mwaka 2014 nikagundua shamba lote limekwisha uzwa na mkata rufaa kabla hata hukumu haijatoka! Nikaenda mahakamni kuulizia kuhusu shauri hili nikaambiwa limekwisha futwa baada ya kukosa mfuatiliaji. Nikafungua mashtaka katika mahakama ya mwanzo kwa kosa la jinai mrufani kuuza shamba kabla ya rufaa kutolewa hukumu! Cha kushangaza mrufani sasa hivi ana hukumu iliyotolewa tarehe 5/2/2015 ikimpa ushindi. Sasa waheshimiwa naomba msaada wenu wa kisheria nafanya nini kuanzia hapa ili kuipta haki yetu? Kwani kwenye mabaraza ya ardhi ya kijiji na kata tulipata ushindi
naombeni msaada ndugu zangu
naombeni msaada ndugu zangu