Naomba msaada wa kumpata huyu mwizi

Naomba msaada wa kumpata huyu mwizi

Ulongupanjala

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2013
Posts
8,273
Reaction score
13,567
Juzi kuna rafiki yangu kutoka Urusi alifikia Chelsea Hotel iliyopo Lumumba street,Dar salaam.

Alikutana na watu nje ya hoteli wakamshawishi kuwa watampa huduma ya usafiri wa kwenda airport siku inayofiata, siku ya juzi baada ya kuingia kwenye gari yao wakiwa wawili walivyoenda umbali kidogo wanaongezeka tena watu wawili na kuanza kumnyang'anya vitu vyake jamaa alipambana nao na wakafanikiwa kumnyang'anya camera yake aina ya Sonny na saa ya mkononi.

Ninayo namba ya simu ya mmoja wa wezi hao ambayo alikuwa anachati na rafiki yangu. Rafiki yangu tayari ameshaondoka Tanzania lakini ana uhitaji mkubwa. Wa kupata vitu vyake. Video ya mmoja wa hao wezi hiyo hapo.

Tukio limetokea jana asubuhi around 10:00
Anaweza kunisaidia kupata hivyo vitu zawadi nono itatolewa.

Asante.
 
Huyo rafiki yako nae ni mburula alishindwa kukariri plate namba ya ilo gari?
 
Nenda Police kafungue kesi- kisha wataitrack hiyo namba na pia kwenye call log ya hiyo namba kutakuwa na namba alizokuwa anapiga/Kupigiwa- apo mtapata washirika wake wote na yeye.
 
Huyo kibaka mwenyewe mbona kachoka hivyo. Ndio maana walishindwa kumpora vitu vingi.

Na hayo mazingira mbona yamekaa kama vilabu vya uswazi, itakuwa mrusi alitaka kuonja papa ya kienyeji akaishia mikononi mwa mipapa dume iliyotaka kumpurusia mali zake.
 
Nakupa sehemu mbili za kumpata mwizi wako .

Jitahidi uwe unaenda makao makuu ya Gal sport Tz pale kwenye jengo la KFC pale fire ingia wanakobetia huyu mwizi wako ni mshirika mzuri hasa mida ya mchana na jioni yuko pale .

Ukimkosa hapo nenda mtaa wa pemba kariakoo sitaki kukueleza direct nyumba ipi wala sehemu ipi ila uliza wanapouza gomba /mirungi utamkuta hapo anasaga mida ya saa saba mpaka saa tisa ndiyo mida yake .

Pole sana , ila jua mwizi wako ni teja lakini pia ana hali ngumu hivyo ikikupendeza msamehe tu
 
Polisi watakulia wewe hela zako na wakiwakamata hao vibaka nao wataliwa hela zao.

Wewe ndiye utapoteza zaidi.
 
kwa urasimu uliojaa nchi hii ni bora upotezee tu hasa ikizingatiwa muhisika hayupo.

Mipolisi ilivyo na njaa hata hao jamaa wakikamatwa wataishia kuchukuliwa hivyo vitu waachiwe tu.

Hili jambo linatuaibisha sana kama Wa Tz tukiwa na watu wengine wasio wa hapa, hawaelewi polisi wetu.
 
Mwambie akaripoti wizara yao ya mambo ya nje wao watawasiliana na balozi ya Tanzania Huku wakipewa namba yako hao wezi watapatikana au awasiliane na ubalozi wao ulioko Huku watapata majibu
 
Back
Top Bottom