Naomba msaada wa kusaidiwa kupata masomo

jasmineisaack

New Member
Joined
Aug 17, 2024
Posts
4
Reaction score
7
Hello habari,

Samahan mimi ni binti nina miaka 24 nilihitimu kidato cha nne mwaka 2018 lakini sikubahatika kuendelea na masomo kutokana na hali ngumu ya nyumbani japo matokeo yangu yaliruhusu kuendelea

Nimepitia changamoto nyingi hapa kati lakini mwaka jana nikakutana na baba yangu mdogo tuliepotezana nikiwa shule ya msingi akaniahidi kunisomesha na ilibidi mwaka huu niingie chuo nisome diploma in social work lakini kwa bahati mbaya alifariki mwezi mmoja nyuma

Alikuwa ni mmoja kati ya wale madaktari wawili waliofariki NJOMBE kwa ajali ya pikipiki hvyo nimebaki sina tegemeo lingine.

Naomba kupitia JamiiForums nipate msaada kama kuna shirika linafahamika linaweza kunisaidia nifikie ndoto yangu maana hali ya nyumbani ni ngumu sana.

Asante
 
Pole Sana madam,. Ngoja waje kukupa muongozo
 
Pole Sana , MUNGU akusimamie ushuri Kama upo Bukoba nenda ofisi ya mh Mbunge umpelekee ombi lako naimani watakusaidia ujuzi wowote


Mungu akusimamie 🙏🏽
 
Mimi mdogo wangu naweza kukusaidia nafasi ya kazi kwa Dodoma,na kwa kuwa Dodoma kuna Vyuo vingi kama CBE,Mipango, UDOM nk,nashauri jaribu kuingia kwenye Website ya hivyo Vyuo uone Course gani unaweza kuisoma,ili kama ina Evening Classes basi asubuhi mpaka mchana unakuwa kazini,kisha saa 9 unaingia darasani. Kupata mtu binafsi wa kukusomesha moja kwa moja ni mtihani ataishia kutaka return ya Uchi tu. Na kupata Taasisi ya kukusomesha moja kwa moja ni process ndefu pia.
Na nikuulizie tangu 2018 mpaka hii 2024 ulikuwa wapi kuomba msaada??au ulikuwa umeolewa??maana kuanza Certificate ukiwa na miaka 24 nayo ni changamoto mdogo wangu
 
Ntashukuru sana hata kwa msaada wa kazi, ndio hapa kati nilipitia changamoto nyingi sana. Pia nina certificate ya computer application. Namba yangu ni 0653840781
 
Ntashukuru sana hata kwa msaada wa kazi, ndio hapa kati nilipitia changamoto nyingi sana. Pia nina certificate ya computer application. Lakini pia kazi yoyote nipo tayari kujifunza na kuifanya npo tayari kuface any challenges.
WhatsApp number ni 0710891683
 
Tuwasiliane huenda nikakusaidia.0787661973
 
Achana na ndoto za alinacha social work ndio mdudu Gani ungekuja tu tuowane Elimu yenyewe ni kitapeli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…