Naomba msaada wa sheria ya ndoa

jaflex

Member
Joined
Mar 3, 2011
Posts
15
Reaction score
3
Hivi ukimtole mwanamke mahali na umezaa nae baada ya hapo mkakosana na kutenge je anahaki ya kuomba talaka? na kuhusu mtoto ninahaki ya kumchukua baada ya muda gani mtoto mwenye now ana mwaka mmoja.naomba kuwasilisha
 
Ndoa ipi? ya kiislamu, kikristo, kiserikali au ya jadi?Ninavyojua kuna imani zingine ambazo ndoa ikifungwa ni kifo tu ndiyo kinawatenganisha.
 
Duh. Kwani hakuna njia yoyote unayoweza kurekebisha masuala haya?
 
sasa hapo si hakuna ndoa mliyofunga?kuhusu mtoto mbona bado mdogo?
 
haijafungwa ndoa ni mahali tu ndio iliyotolewa ndoa haikufiwa
 
ndio mkuu hakuna ndoa ila kinacho nishangaza huyu mwanamke anaongelea talaka sasa nilitaka kujua labda kisheria yuko sahihi au la
 
Hivi ukimtole mwanamke mahali na umezaa nae baada ya hapo mkakosana na kutenge je anahaki ya kuomba talaka? na kuhusu mtoto ninahaki ya kumchukua baada ya muda gani mtoto mwenye now ana mwaka mmoja.naomba kuwasilisha
Mkuu Jaflex, kwa mujibu wa sheria ya ndoa ya mwaka 1971, kuzaa tuu na mwanamke sio ndoa, au kumtolea tuu mahari hata kama mmezaa nae pia sio ndio, huko kunaitwa uchumba!.

Uchumba unaweza kuvunjika wakati wowote na hauna talaka, ila uchumba ukivunjika, zile mahari na zawadi ulizopeleka rasmi, zingeweza kurudishwa kama hakukuwa issue (issue hapa ni mtoto), lakini kwa vile tayari kuna issue, hata hizo mahari hazirudishwi!.

Baada ya kuvunjika kwa uchumba wenye mtoto, wewe sasa unawajibika kutoa matunzo ya kumlea huyo mtoto, na kwa mujibu wa sheria, "hiyo ya 1971" ambayo sikumbuki kama imeishabadilishwa, unapaswa kutoa matunzo ya shilingi mia moja kwa kwa mwezi kwa kila mtoto!.

Ila kama huyo mwanamke, mmeishi nae nyumba moja, kwa kipindi cha miaka 2, hadi kumzaa huyo mtoto!, then kumuacha hivi hivi, japo hana talaka rasmi kwa sababu hakuna ndoa rasmi liyofungwa, lakini anastahili haki zote za mke, ikiwamo kugawana mali mlizochuma wote!, hata kama yeye alikuwa ni golikipa tuu!.

Pasco.
 
Ndoa ipi? ya kiislamu, kikristo, kiserikali au ya jadi?Ninavyojua kuna imani zingine ambazo ndoa ikifungwa ni kifo tu ndiyo kinawatenganisha.
Sheria ya ndoa inatambua misingi ya dini katika kuunganisha waumini wao yaani kuwashawishi na kuwafungisha ndoa kwa niaba ya serikali .Hivyo shehe au padri akifungisha ndoa lazima awe na kibali kutoka mamlaka husika.tofauti na hapo ndoa inakuwa Void.

Kuhusu suala la kutengana ni mahakama tuu yenye uwezo wa kutenganisha ndoa.Hii inafuta kabisa dhani za Kikristo kwamba ndoa haitenganishwi na dhana ya kiislamu ya talaka rejea na nyinginezo kwani kisheria hazitambuliki.Ninamaliza kwa kusema kuwa ni mahakama tuu yenye uwezo wa kutenganisha ndoa baada ya kuona kuwa yapaswa kufanya hivyo kuokana na hali iliyopo na haikubaliani na vigezo vya kidini kuwa ndoa hazitenganishwi.
 
hapo kaka umenisaidia nimekuele sana
 
Mkuu hesima kwako. naomba nitofautiane kidogo nawewe hapo kwenye red. Ni kweli kabisa mahari ni sehehu ya uchumba lakini kuzaa Mtoto haipo kabisa kwenye harakati za uchumba. kuzaa mtoto na mchumba wako hubadilika na kuwa ama ndoa iliyojifunika kwenye kimvuli cha DHANA YA NDOA (PRESUMPTION OF MARRIAGE) au Uasherati. kwa kiswahili cha sasa ungeseama kijana kuzaa na mchumba wake kabla ya ndoa AMEHARIBU ndio maana makabila mengi ikitokea hivyo mchumba anapigwa faini
 
sasa wakuu mmejbu vyema ila nna swali hapo...
hv mwanaume aliyezaa hvyo katka uchumba na msichana na hatoi matunzo kwa mtoto na mama wa mtoto kama sheria inavosema nn adhabu yake...?? kisheria mahakamani...

Maana hii imemkuta mdogo wetu anapata tabu sana kulea kichanga chake na yeye hana kazi
Nn cha kufanya wakuu??
 
Halafu walkuu vp kuhusu milki ya mtoto ni mali ya mwanamke au mwanamme? pale wanapotengana pasipo ndoa.(uchumba)

Na je ni mda gan hasa mtoto anatakiwa kwenda kwa babake rasmi.
 
mahakama ya Tanzania? au the hague? Ulishawahi kusikia mahakama imevunja ndoa ya mtu? au umeshawahi kusikia mahakama imewaamuru watu kufunga ndoa?
 
ndio mkuu hakuna ndoa ila kinacho nishangaza huyu mwanamke anaongelea talaka sasa nilitaka kujua labda kisheria yuko sahihi au la
Hapo hakuna ndoa.sheria inasema mtoto atakaa chini ya uangalizi wa mama yake mpaka atimize miaka 7.
 
mahakama ya Tanzania? au the hague? Ulishawahi kusikia mahakama imevunja ndoa ya mtu? au umeshawahi kusikia mahakama imewaamuru watu kufunga ndoa?
Mkuu mahakama yoyote ya Tanzania haina mamlaka ya kufungisha ndoa. Serikali hufungisha ndoa kupitia ofisi ya mkuu wa wilaya na watu wengine waliopewa kibali kufungisha kwa niaba ya serikali kama mapadre , baadhi ya mashehe na wachungaji mkuu.

Kuhusu suala la kuvunja ndoa mkuu ni kweli kwa mujibu wa sheria ya ndoa ya Tanzania ni mahakama pekee yenye mamlaka ya kuvunja au kutengua ndoa na kutoa kibali ambacho kinawaweka huru waliokua wanandoa hao kiitwacho certificate of divorce.Lakini mkuu kabla mahakama haijatengua ndoa lazima upitie hatua ngumu sana na sheria imeweka ugumu huo makusudi ili kutimiza sharti kuu la ndoa la kuishi milele yote mpaka kifo kiwatenganishe na hii ipo wazi kwenye sehemu ya 9 ya sheria ya ndoa ya mwaka 1971.

Hata hivyo mkuu kama mahakama itajiridhisha kwamba uhusiano wa wanandoa hao hauwezekaniki tena na ikiendelea kungangania waishi pamoja maafa kama kifo na vilema na mengine yanayofanana na hayo yaweza kuokea ,kisherea wanasema ndoa imepasukapasuka na haina kipuli cha kuweza kuitengeneza( marriage has broken down irreparably) basi mahakama itavunja ndoa hiyo
 
ulichokifanya umeconcubine, kuishi maisha ya uasherati. Lakini kwa kipindi hicho chote mlichokaa mmepata hadhi ya mke na mme. Kwa vile mnataka kutengana, mke atapata haki zote kama mwanandoa baada ya mahakama kuwatenganisha kisheria "separation" na kisha kutamka mgawanyo halali wa mali mlizochuma pamoja na majukumu ya kumlea mtoto yatakapoangukia ambapo mara nyingi huwa ni kule ambako mtoto atapata ustawi bora ( basing on the best interest of the child).

Kwa kuanzia ushauri huu unaweza kusaidia.
 
Mkuu pole sana hapa ndio sheria inapokuwa na kichefuchefu kuhusu hao malaika wasio na hatia.Kanza sheria inamuita illegitimate child kwa kiswahili lanishinda kutafsiri au wakati mwingine huitwa child born out of wedlock. Huyu mtoto sheria inamgandamiza sana. Sheria inayozungumzia haki za huyu mtoto inaitwa Affiliation act na huyo baba yake huitwa putative father

Sasa basi ni jukumu la mwanadada aliyepewa mimba na mtu anayedai kuwa ndiye Baba wa mtoto kwenda mahakamani wakati akiwa mjamzito au miezi 12 baada ya kujifungua kudai matunzo ya mtoto.

Mahakama itafungua shauri liitwalo affiliation proceeding na kutoa samasi kumuita huyo anayedhaniwa kuwa baba wa huyo mtoto. ushahidi ukionyesha kweli kuwa ni wa kwake itaamuru kutoa garama za kujifungua na matunzo ya mtoto kwa mwezi ambayo zamani ilikuwa ni dola za kimarekani 0.1 kwa mwezi sasa hivi sijui watu wa ustawi wa jamii waweza kukusaidia

Mtoto wa namna hii huitwa kwa jina la babu yake na kama huyo baba atamuitaji kuna kiasi fulani anatakiwa amlipe babu yake na hii ni kwa mujibu wa sheria inayohusu hali za watu.lakini kiwango hicho ni kidogo sana na ili mtoto asiitwe tena wa nje ya ndoa hufanyika kataratibu kama cha kum adopt


 
Ninacho faham kumchukua mtoto kutoka kwa mama ni miaka 7, lakini kamaitaonekana hatapata haki stahili utapewa akiwa na miaka 18. naikionekana kwa mama nako hatapata matunzo mazuri utapewa baada ya kuachishwa ziwa{kunyonya}
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…