Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu Jaflex, kwa mujibu wa sheria ya ndoa ya mwaka 1971, kuzaa tuu na mwanamke sio ndoa, au kumtolea tuu mahari hata kama mmezaa nae pia sio ndio, huko kunaitwa uchumba!.Hivi ukimtole mwanamke mahali na umezaa nae baada ya hapo mkakosana na kutenge je anahaki ya kuomba talaka? na kuhusu mtoto ninahaki ya kumchukua baada ya muda gani mtoto mwenye now ana mwaka mmoja.naomba kuwasilisha
Sheria ya ndoa inatambua misingi ya dini katika kuunganisha waumini wao yaani kuwashawishi na kuwafungisha ndoa kwa niaba ya serikali .Hivyo shehe au padri akifungisha ndoa lazima awe na kibali kutoka mamlaka husika.tofauti na hapo ndoa inakuwa Void.Ndoa ipi? ya kiislamu, kikristo, kiserikali au ya jadi?Ninavyojua kuna imani zingine ambazo ndoa ikifungwa ni kifo tu ndiyo kinawatenganisha.
hapo kaka umenisaidia nimekuele sanaMkuu Jaflex, kwa mujibu wa sheria ya ndoa ya mwaka 1971, kuzaa tuu na mwanamke sio ndoa, au kumtolea tuu mahari hata kama mmezaa nae pia sio ndio, huko kunaitwa uchumba!.
Uchumba unaweza kuvunjika wakati wowote na hauna talaka, ila uchumba ukivunjika, zile mahari na zawadi ulizopeleka rasmi, zingeweza kurudishwa kama hakukuwa issue (issue hapa ni mtoto), lakini kwa vile tayari kuna issue, hata hizo mahari hazirudishwi!.
Baada ya kuvunjika kwa uchumba wenye mtoto, wewe sasa unawajibika kutoa matunzo ya kumlea huyo mtoto, na kwa mujibu wa sheria, "hiyo ya 1971" ambayo sikumbuki kama imeishabadilishwa, unapaswa kutoa matunzo ya shilingi mia moja kwa kwa mwezi kwa kila mtoto!.
Ila kama huyo mwanamke, mmeishi nae nyumba moja, kwa kipindi cha miaka 2, hadi kumzaa huyo mtoto!, then kumuacha hivi hivi, japo hana talaka rasmi kwa sababu hakuna ndoa rasmi liyofungwa, lakini anastahili haki zote za mke, ikiwamo kugawana mali mlizochuma wote!, hata kama yeye alikuwa ni golikipa tuu!.
Pasco.
hapo kaka umenisaidia nimekuele sana
Mkuu hesima kwako. naomba nitofautiane kidogo nawewe hapo kwenye red. Ni kweli kabisa mahari ni sehehu ya uchumba lakini kuzaa Mtoto haipo kabisa kwenye harakati za uchumba. kuzaa mtoto na mchumba wako hubadilika na kuwa ama ndoa iliyojifunika kwenye kimvuli cha DHANA YA NDOA (PRESUMPTION OF MARRIAGE) au Uasherati. kwa kiswahili cha sasa ungeseama kijana kuzaa na mchumba wake kabla ya ndoa AMEHARIBU ndio maana makabila mengi ikitokea hivyo mchumba anapigwa fainiMkuu Jaflex, kwa mujibu wa sheria ya ndoa ya mwaka 1971, kuzaa tuu na mwanamke sio ndoa, au kumtolea tuu mahari hata kama mmezaa nae pia sio ndio, huko kunaitwa uchumba!.
Uchumba unaweza kuvunjika wakati wowote na hauna talaka, ila uchumba ukivunjika, zile mahari na zawadi ulizopeleka rasmi, zingeweza kurudishwa kama hakukuwa issue (issue hapa ni mtoto), lakini kwa vile tayari kuna issue, hata hizo mahari hazirudishwi!.
Baada ya kuvunjika kwa uchumba wenye mtoto, wewe sasa unawajibika kutoa matunzo ya kumlea huyo mtoto, na kwa mujibu wa sheria, "hiyo ya 1971" ambayo sikumbuki kama imeishabadilishwa, unapaswa kutoa matunzo ya shilingi mia moja kwa kwa mwezi kwa kila mtoto!.
Ila kama huyo mwanamke, mmeishi nae nyumba moja, kwa kipindi cha miaka 2, hadi kumzaa huyo mtoto!, then kumuacha hivi hivi, japo hana talaka rasmi kwa sababu hakuna ndoa rasmi liyofungwa, lakini anastahili haki zote za mke, ikiwamo kugawana mali mlizochuma wote!, hata kama yeye alikuwa ni golikipa tuu!.
Pasco.
mahakama ya Tanzania? au the hague? Ulishawahi kusikia mahakama imevunja ndoa ya mtu? au umeshawahi kusikia mahakama imewaamuru watu kufunga ndoa?Sheria ya ndoa inatambua misingi ya dini katika kuunganisha waumini wao yaani kuwashawishi na kuwafungisha ndoa kwa niaba ya serikali .Hivyo shehe au padri akifungisha ndoa lazima awe na kibali kutoka mamlaka husika.tofauti na hapo ndoa inakuwa Void.
Kuhusu suala la kutengana ni mahakama tuu yenye uwezo wa kutenganisha ndoa.Hii inafuta kabisa dhani za Kikristo kwamba ndoa haitenganishwi na dhana ya kiislamu ya talaka rejea na nyinginezo kwani kisheria hazitambuliki.Ninamaliza kwa kusema kuwa ni mahakama tuu yenye uwezo wa kutenganisha ndoa baada ya kuona kuwa yapaswa kufanya hivyo kuokana na hali iliyopo na haikubaliani na vigezo vya kidini kuwa ndoa hazitenganishwi.
Hapo hakuna ndoa.sheria inasema mtoto atakaa chini ya uangalizi wa mama yake mpaka atimize miaka 7.ndio mkuu hakuna ndoa ila kinacho nishangaza huyu mwanamke anaongelea talaka sasa nilitaka kujua labda kisheria yuko sahihi au la
Mkuu mahakama yoyote ya Tanzania haina mamlaka ya kufungisha ndoa. Serikali hufungisha ndoa kupitia ofisi ya mkuu wa wilaya na watu wengine waliopewa kibali kufungisha kwa niaba ya serikali kama mapadre , baadhi ya mashehe na wachungaji mkuu.mahakama ya Tanzania? au the hague? Ulishawahi kusikia mahakama imevunja ndoa ya mtu? au umeshawahi kusikia mahakama imewaamuru watu kufunga ndoa?
Mkuu pole sana hapa ndio sheria inapokuwa na kichefuchefu kuhusu hao malaika wasio na hatia.Kanza sheria inamuita illegitimate child kwa kiswahili lanishinda kutafsiri au wakati mwingine huitwa child born out of wedlock. Huyu mtoto sheria inamgandamiza sana. Sheria inayozungumzia haki za huyu mtoto inaitwa Affiliation act na huyo baba yake huitwa putative fathersasa wakuu mmejbu vyema ila nna swali hapo...
hv mwanaume aliyezaa hvyo katka uchumba na msichana na hatoi matunzo kwa mtoto na mama wa mtoto kama sheria inavosema nn adhabu yake...?? kisheria mahakamani...
Maana hii imemkuta mdogo wetu anapata tabu sana kulea kichanga chake na yeye hana kazi
Nn cha kufanya wakuu??