Hii mada na yanayojadiliwa hapa ni udhalilishaji wa kina mama zetu. Sifahamu watu mna matatizo gani, nchi ina mambo mengi sana ya kimsingi ya kujadili lakini watu mnapoteza muda kwenye mambo yasiyo ya kimsingi tena kuwadhalilisha hawa waliotuzaa, hivi kweli unapoleta mada kama hii huwa unafikiria kweli kuwa una mama, dada, shangazi, fikiria kuwa unmwambia kati ya hao kabla ujaleta mada yako ya hovyo kabisa. Hata kama ni kuburudisha watu kuna mambo ya jokes na yakuchekesha mengi tu, kwanini wanaume tunaendelea kuwadhalilisha kina mama kwa tungu na majina ya dhihaki, hadi lini? hakuna mambo ya kuwasifia hawa kina mama kwenye jamii hii yetu.