Naomba msaada wa wakili mzuri aliyepo Sengerema, Mwanza atakayeweza kusaidia hili suala la NMB kugoma kutoa hati ya mteja wao kwa miaka mitano

Nyabukika

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2022
Posts
1,440
Reaction score
1,046
Ndugu zangu naomba tumsaidie huyu mama anayezungushwa na NMB kupewa hati yake aliyoitumia kama dhamana ya mkopo miaka 5 iliyopita.

Naomba msaada wa kisheria kama kuna wakili humu ambaye yuko Sengerema, Mwanza anaweza kusimamia hili suala.

NB: MKOPO UMESHALIPWA MIAKA 5 ILIYOPITA

Pia soma: Yule mama amerejeshewa hati yake iliyokaa bank ya NMB kwa miaka 5
 
Hahaha!! Dawa ya mkopo ni kulipa. Mwambie alipe deni sw.

KAZI ni kipimo cha UTU
 
Hapo haujaelewa nini mkuu mkopo umeshalipwa miaka 5 iliyopita niliweka kwenye post iloyopita sasa baada ya wadau wengi kushauri ndio maana tunaomba msaada ya kisheria
 
Ndugu zangu naomba tumsaidie huyu mama anayezungushwa na NMB kupewa hati yake aliyoitumia kama dhamana ya mkopo miaka 5 iliyopita.

Naomba msaada wa kisheria kama kuna wakili humu ambaye yuko Sengerema, Mwanza anaweza kusimamia hili suala.
Uzi wako wa mwanzo wa tatizo ungeuambatanisha hapo chini.
 
Sababu wanazotoa NmB ya kushindwa kuirudisha hati ni nini?? Wameipoteza? Na kuna mtu mwingine tofauti na yeye ambaye anaitumia kama dhamana kinyume cha Taratibu??
 
Wanamwambia "nenda nyumbani tutakupigia simu" na taratibu zote za kuandika barua kwa ajili ya kuomba hati ameandika
 
Hapo haujaelewa nini mkuu mkopo umeshalipwa miaka 5 iliyopita niliweka kwenye post iloyopita sasa baada ya wadau wengi kushauri ndio maana tunaomba msaada ya kisheria
Aende dawati la jinsia
 
Anza na TAKUKURU kwanza
 
Cheki na Wakili Bernard Otieno yupo Geita hapo atakusaidia chapu
 
Hapo haujaelewa nini mkuu mkopo umeshalipwa miaka 5 iliyopita niliweka kwenye post iloyopita sasa baada ya wadau wengi kushauri ndio maana tunaomba msaada ya kisheria
mpigie Huyu Advocate 0715450012 wa Mwanza anayafahamu haya mambo ya commercial laws.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…