Fungua GENGE; kama upo DAR nenda asubuhi kariakoo nunua vitu kwa jumla halafu unakuja kuuza mtaani kwako. Tengeneza mazingira mazuri ya biashara, ikiwezekana weka huduma ya kupeleka bidhaa nyumbani kwa mteja. Tafuta wateja wa kudumu hapo mtaani kwako kwa kuwatembelea na kuwaeleza adhima yako ya kuwaletea bidha za jikoni kama nyanya, vitunguu n.k. kisha tafuta kijana ambae utampatia baiskeli halafu asubuhi anapita kwa wateja wako kuchukua order ya mahitaji yao na baadae kuwasambazia.