Wakuu natumai nyote muwazima naombeni msaada mimi ni mkulima ninaemiliki shamba mkoani Tanga wilaya ya kilindi kijiji cha masagusa, nimekuwa nikisumbuliwa mara kwa mara na wafugaji jamii ya wamaasai na malalmiko yangu nilijaribu kuyapeleka kwenye ofisi ya kijiji lakini hadi sasa ninapoandika uzi huu ofisi hyo imeshindwa kuwawajibisha hao wafugaji, mwezi uliopita walimpiga kijana wangu wa shamba na nilifika kutoa taarifa ofisi ya kijiji lakini hakuna walichokifanya zaidi ya kunizungusha zungusha na bila msaada wowote, hii tabia imekuwa mbaya kwani wamaasai hao imefikia hatua wanajiona wao wana haki juu ya maeneo ya wakulima ili hali wao wametengewa maeneo yao yamalisho ambayo hawataki kwenda. kiukweli hili swala linaumiza na linaudhi sana unakuta mtu shambani umepanda mazao yako ambayo ndo unategemea uvune uuze ulipie ada ya watoto pamoja na chakula halafu wanakuja watu wanachungia kwenye mazao yako bila kujali ni gharama kiasi gani umetumia hapo, hivyo kwakuwa huku kuna wadau wengi nina imani nitapata msaada wa kiushauri lakini pia na kisheria ili nikomeshe tabia hii. Naombeni msaada wenu wakuu Asanteni.