naomba msaada wakisheria tafadhari

Homa la jiji

Senior Member
Joined
Jan 13, 2014
Posts
129
Reaction score
28
Mimi niliolewa na mme wangu miaka kumi iliopita tulianza maisha tukiwa jijini mbeya tuliyaanza maisha tukiwa tunafanya biashara ndogo ndogo atimae tukaanza kufanya biashara kubwa na atimae tukahamia jijini dar hapo tukapata mafanikio makubwa ambayo yalijionyesha kwa jamii na mme wangu alikua amekua akifungasha mzigo mara mbili kwa mwezi nchini china na ilipofikawezi wa tatu mwaka jana tulipata zarura yakuuguliwa na mama yangu mzazi ikabidi niende kumjulia hali yeye mmewangu akadai atakuja huko mby nilipokaa siku kadhaa nikampigia simu kua mama kapata nafuu mitarudi keshokutwa akasema usirudi mpaka nitakapo kujulisha nikashtuka zilipofika siku mbili mbele nikamuona shemeji yangu na mshenga wakija kwa wazazi wangu wakaleta barua na sh. Mlioni moja barua ilimtaka baba anipokee mpaka atakapo kuja kunichukua nakuanzia hapo akawa hapokei cm yangu wala kujibu meseji niliamua kuja hapa dar nilipofika ndani kwangu nikakuta mme wangu ameoa mke mwingine na kamuweke nyumbani kwangu na kitanda ninacholalia ndipo alinifukuza kama mbwa nikaenda kulala kwa dada angu ambae anaishi hapa dar nililala huko asubuhi nikashauriwa kwenda kituo cha haki za binadamu kinondoni alipoitwa mme wangu tukatoa maelezo ikabidi niambiwe naipeleke shauri langu ustawi wa jamii nilipo toka pale mme wa dada angu akaniambia twende tukashauri swala hili akaniambia nipande kwenye gari lake tukaelekea maeneo ambayo siyajui huko nikaingizwa kwenye nyumba moja nakumkuta mme wangu na wababa wengine wawili wakafunga mlango nakunishawishi nirudi mbeya nawakaniambia nipokee milioni sita nilipoonyesha msimamo wangu walinitishia kwa kauli mbalimbali knikaogopa nakupokea milioni sita nawakaniandikia barua yenye muhuri wa mwenyekiti wakitongoji hicho kua nimepokea mgao wa mali tulizochuma nawakati tumechuma mali nyingi na nyumba tumejenga maduka mawili moja kariakoo jingine tunduma mbeya ilibidi niende kuwajulisha wazazi kwakitendo nilichofanyiwa hivi nimerudi kwa dada angu amenipeleka ustawi wa jamii na mme wangu ameitwa hivi kesho tunatakiwa tufike huko lakini huyu bwana ameshanipigia cm zaidi ya mara kumi akisema hawezi kuukuja na atanunua mawakili watano ili anishinde nahitaji msaada wakisheria
 
A contract becomes voidable when the consent of one or more of the parties to a contract is obtained by coercion, undue influence, misrepresentation or fraud an agreement which is enforceable by law at the option of one or more parties but not at the option of the other or others is a voidable contract.

Mimi si mwanasheria lakin nilisoma business law/law of contract kwa kipengere hiko cha hapo juu hata kama ulisign but hicho kitu bado kina kupa haki ya wewe kujitetea kwani ulisign kwa lazima(coercion).chamsingi kesi kama hii tafuta mwanasheria tu,atakupa msaada zaidi,i hope mungu atasaidia pia
 
Pole sana dada yetu,ninachokuomba au kukushauri tafta mwana sheria atakusaidia maana haki yako bado haija potea hapo amekuonga au kukupa rushwa ambayo ni kosa kisheria.Haki yako bado ipopalepale endapo hautakata tamaa.
 
Wanasheria watano hawana uwezo wa kupoteza haki yako, fight for it madam ila inapaswa uwe na ushahidi wa kutosha...
 
Hapo kunamambo mawili lazima ufahamu:
1. No extra judicial Divorce. Hakuna talaka inayoweza kutolewa na Mamlaka yeyote isipokuwa Mahakama.
2.Mgawanyo wa Mali unapofanyika ni lazima uzingatie Haki usawa na mchango wawanandoa katika kuhakikisha mgawanyo sawa wa mali ambazo utathibitisha kwamba ni mchumo wa ndoa.
3.Siyo kila Mali iliyopo inaweza kugawanywa kwa hiyo ni vema uangalie ni mali ipi na uandae ikiwemo kutunza kumbukumbu ya namna ulivyoshiriki katika kutunza na kuendeleza mali hiyo.
4.Hiyo milioni sita uliyopokea isikupe hofu ni sehemu ya haki yako ya matunzo katika kipindi hiki ambacho haukuwa kwenye ndoa ukizingatia kwamba ulipewa fedha hizo siyo kwa ridhaa na makubaliano bali kwa shinikizo .
5.Hiyo ndoa aliyofunga Mumeo na huyo mwanamke ni haramu na ni kosa lajinai ukiwashtaki vilevile wanaweza kufungwa miaka Miwili

FANYA YA FUATAYO:
1.Iwapo unafikiri huwezi kuendelea na Ndoa hiyo nenda Ustawi wa Jamii na uombe barua ya kushindwa kwa
usuluhishi.
2.Nenda katika Mahakama ya Mwanzo au Mahakama Kuu na kuwasilisha ombi lako la Talaka.
3.Katika ombi lako ambatisha orodha ya mali zote unazo dai pamoja na amadai ya matunzo mpaka utakapoolewa
au kupata namana ya kujitegemea
4.Katika Maelezo yako hujaeleza iwapo muna watoto katika ndoa yenu , iwapo wapo kutegemeana na umri wao Omba amri ya Ulezi na
Matunzo ya watoto yawe kwa baba kwa kiwa ngo kilekile walichopewa kabla ya ndoa yenu kutetereka na kuvunjika.
Ushauri huu ni wa Jumla hivyo usiutegemee pekee, tafuta Mwanasheria aliye karibu nawe ili aweze kukusaidia na kukupa maelekezo vema kwa gharama zako.
 
Hizo milioni 6 alizokupa kamkodie majambazi wamrudishe mbinguni halafu rudi kachukue mali zako. Jasho la mtu haliliwi.

Sent from my Nokia Lumia using Tapatalk
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…