Homa la jiji
Senior Member
- Jan 13, 2014
- 129
- 28
Mimi niliolewa na mme wangu miaka kumi iliopita tulianza maisha tukiwa jijini mbeya tuliyaanza maisha tukiwa tunafanya biashara ndogo ndogo atimae tukaanza kufanya biashara kubwa na atimae tukahamia jijini dar hapo tukapata mafanikio makubwa ambayo yalijionyesha kwa jamii na mme wangu alikua amekua akifungasha mzigo mara mbili kwa mwezi nchini china na ilipofikawezi wa tatu mwaka jana tulipata zarura yakuuguliwa na mama yangu mzazi ikabidi niende kumjulia hali yeye mmewangu akadai atakuja huko mby nilipokaa siku kadhaa nikampigia simu kua mama kapata nafuu mitarudi keshokutwa akasema usirudi mpaka nitakapo kujulisha nikashtuka zilipofika siku mbili mbele nikamuona shemeji yangu na mshenga wakija kwa wazazi wangu wakaleta barua na sh. Mlioni moja barua ilimtaka baba anipokee mpaka atakapo kuja kunichukua nakuanzia hapo akawa hapokei cm yangu wala kujibu meseji niliamua kuja hapa dar nilipofika ndani kwangu nikakuta mme wangu ameoa mke mwingine na kamuweke nyumbani kwangu na kitanda ninacholalia ndipo alinifukuza kama mbwa nikaenda kulala kwa dada angu ambae anaishi hapa dar nililala huko asubuhi nikashauriwa kwenda kituo cha haki za binadamu kinondoni alipoitwa mme wangu tukatoa maelezo ikabidi niambiwe naipeleke shauri langu ustawi wa jamii nilipo toka pale mme wa dada angu akaniambia twende tukashauri swala hili akaniambia nipande kwenye gari lake tukaelekea maeneo ambayo siyajui huko nikaingizwa kwenye nyumba moja nakumkuta mme wangu na wababa wengine wawili wakafunga mlango nakunishawishi nirudi mbeya nawakaniambia nipokee milioni sita nilipoonyesha msimamo wangu walinitishia kwa kauli mbalimbali knikaogopa nakupokea milioni sita nawakaniandikia barua yenye muhuri wa mwenyekiti wakitongoji hicho kua nimepokea mgao wa mali tulizochuma nawakati tumechuma mali nyingi na nyumba tumejenga maduka mawili moja kariakoo jingine tunduma mbeya ilibidi niende kuwajulisha wazazi kwakitendo nilichofanyiwa hivi nimerudi kwa dada angu amenipeleka ustawi wa jamii na mme wangu ameitwa hivi kesho tunatakiwa tufike huko lakini huyu bwana ameshanipigia cm zaidi ya mara kumi akisema hawezi kuukuja na atanunua mawakili watano ili anishinde nahitaji msaada wakisheria