naomba msaada wenu madaktari

naomba msaada wenu madaktari

Wizzo

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2010
Posts
723
Reaction score
256
jamani nsaidieni ninasumbuliwa na kichefuchefu mate yanajaa mdomoni nahisi kutapka ila sitapiki,nlenda hospital nkaambiwa nna minyoo nkapewa dawa kweli nkaona nafuu ila baada ya wiki 2 tu hali imerudi ileile.nsaidieni tatizo ni nini
 
kama dawa ya hospitali ilikusaidia kiasi, safi. ni indication kwamba dawa ilipunguza tatizo na tatizo ni kubwa kidogo, so; rudi hospitali ileile umweleze dokta maendeleo na jinsi gani dawa ya mwanzo haikusaidia. nadhani atakupa nyingine au kukupa double dozi.

binafsi, pia nakushauri usile vyakula vya mafuta mfano, mayai ya kukaanga, chips, maziwa fresh sana, etc. wewe kula vitu vya kuchemsha, chemsha viazi, nyama(supu), pia viazi choma safi. katika kila kinywaji weka limao kidogo mfano maji, juice etc.
 
labda unaweza kuwa na mimba kapime
Duh mkuu!!! Ushaijua jinsiayake!!

Mada: Tazama aina za chakula unachokula, je unatumia choo aina gani? je unazingatia usafi wa mikono yako kabla ya kula chochote? maana kutumia dawa pekee na ukarudia tabia ya kula uchafu haitosaidia kuondoa tazizo. Tunapeana mikono na watu njiani kisha tunakula karanga na ghasia zingine bila kunawa mikono, haijalishi wala hatuhitaji kujua tuliopena nao mikono wametoka wapi au mikono yao wameitumia vipi.

Pole sana.
 
Pole sana mkuu!
Nashawishika kuwa kweli una minyoo,sasa nadhani hukufuata ushauri wa dose vizuri.
kwanza baada ya wiki mbili ungetakiwa uende tena hospital ukapime au umeze tena dose nyingine kwani minyoo haikai tuu tumboni ina life cycle yake so unaweza kukuta kuna mayai yaliyokuwa kwenye mzunguko ama kwenye misuli au ini so hayo yangeuawa kwa dose ya pili.
USHAURI.
Epuka kula nyama MBICHI hasa za kuchoma,Mbogamboga ambazo siyo well prepared, matunda ambayo hayajaoshwa vizuri,kumbuka kunawa mikona kabla na baada yakula so in short be hygenic.
Get well soon.
 
Ni vizuri urudi hosp. na utoe hayo maelezo
Usipopata ufumbuzi nenda ngazi ya juu zaidi
Bcoz this is the second time is better to see a Dr.(Si kila anaefanya kazi hosp ni Dr.)
 
asanteni jamani kwa ushauri let me do what u hv advised me.mungu awabariki
 
nmerudi hosp nkabidi nipime tena dk akanambia minyoo imeisha kuna amoeba so nmepewa dawa za amoeba ngoja nione impact yake
 
jamani nsaidieni ninasumbuliwa na kichefuchefu mate yanajaa mdomoni nahisi kutapka ila sitapiki,nlenda hospital nkaambiwa nna minyoo nkapewa dawa kweli nkaona nafuu ila baada ya wiki 2 tu hali imerudi ileile.nsaidieni tatizo ni nini

Babu Loliondo na Kikombe chake ni suluhisho la afya yako!
 
labda unaweza kuwa na mimba kapime

hahaha kwani amekwambia yeye ni ke! pengine ni me; basi tumuulize jinsia yake. ila mimi nafikiri pengine minyoo haijakwishwa hivyo ukichanganya minyoo haijaisha, anakula vyakula vya mafuta n.k lazima kichefuchefu kije..

binafsi najijua nikianza tu kusikia kichefuchefu hasa nimalizapo kula najua nina minyoo. Hivyo nikinywa dawa ya minyoo hali inatoweka nakata miaka (uzima Mungu atupao) ingawa wengine wanashauri kila baada ya miezi mitatu unywe dawa ya minyoo. ila mimi nisiyependa kunywa kunywa dawa naona kuwa kuzingatia kanuni za usafi wa vyakula na maji tunayokunywa tunajilinda pia na minyoo.
 
Back
Top Bottom