Naomba mtupe mrejesho mlioenda kufanya usaili wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Aprili 5

" Tuliripoti uwanjani mapema, tukakaguliwa na kupata maelekezo.

Kisha zikafuata taratibu za kawaida, kuitwa majina, kupimwa urefu, afya n.k.

Tukafanya mazoezi halafu tukaenda uwanjani tukapangwa makundi ya watu kumi kumi.

Tukakimbia mbio za mita mia Moja

Katika mbio za mita mia moja wakachukuliwa wa kwanza, wapili na watatu.

Ikafanyika sorting wale waliopita wakae huku wengine huko ingawa Kuna wengine waliokuwa wameshika nafasi nne na tano au sita walichukuliwa, sijui walitumia vigezo gani?

Kuna wengine hawakukimbia kabisa ila walikuwepo upande wa walioshinda.

Mimi nilikuwa namba nne ndio ukawa mwisho wangu wa usahili.

Tulikuwa kama watu elfu Moja hivi. "

Mwisho wa kunukuu.
 
Itakuwa urefu ndio kigezo kilichowatoa watu wengi
 
Duh basi tupo wengi tumepigwa na kitu kizito
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…