Naomba muongozo wa CHADEMA


Ukipata sehemu nimekuita ccm hapa kwenye hii thread basi niambie ili nikachunguzwe akili. I care less kama wewe ni ccm au mpinzani. Kuna wana ccm hapa kibao tu na tuko nao kwenye mapambano ya kukomboa nchi yetu.

Unavyosema kuwa nendeni vijijini unataka nani akufanyie kazi on your behalf? kwa nini usiseme kuwa twendeni vijijini? kwa nini wewe usiwe sehemu ya haya mapambano?
 

kwani wewe hujulikani hapa?mtu akikosoa chadema kidogo tu basi balaa!!hao wana ccm kibao unaoshirikiana nao kina nani zaidi ya kuwananga?
ninaposema nendeni vijijini namaanisha CUF,CHADEMA,TLP nk waende nao wakaweke mizizi huko siyo kusubiri wakati wa chaguzi tu.
Bahati mbaya siwezi kuwa huko kwa sasa,lakini nilishawahi kuwa muhamasishaji wa vijana katika kampeni ya ubunge ya jamaa mmoja wa upinzani,2005.nway jimbo lilikuwa wazi kabisa lakini jamaa hakushinda kwa mikakati mibovu ya chama chake.Kwahiyo naweza kusema kamchango kangu kali play part fulani siku zile na naamini kama 2010 atakwenda mpinzani makini na ccm wakampitisha yule mzee,basi watang'oka.
Nadhani unaipata falsafa yangu sasa.Siyo Chadema wala CCM ila siku zote nita support kiongozi makini na siyo hawa waganga njaa!
 


"Kuna nini ambacho kipo CCM ambacho huwezi kukipata katika Upinzani" ?

hilo swali lako! Unajua mkuu tunatofautiana padogo sana.Huyu Shayo ni mfano tu na ndiyo upinzani wa tanzania ulivyo.Ubinafsi,unafiki,umamluki,mizengwe,kuwekeana vikwazo wao kwa wao nk
mimi sifurahii maovu yanayofanywa na watu wa ccm.hoja yangu ni kwamba wakati umefika sasa Kwa tanzania kuwa na chama makini kabisa na chenye nguvu za kuweza kuikabili ccm.Siyo huu utitiri usiyo na kichwa wala miguu na kila mtu kugombea urais hali akijua kabisa kuwa hatopata.
nadhani sasa umenipata!
 
kwani wewe hujulikani hapa?mtu akikosoa chadema kidogo tu basi balaa!!hao wana ccm kibao unaoshirikiana nao kina nani zaidi ya kuwananga?

Wewe unategemea mtu akosoe Chadema au wapinzani bila sababu ya kueleweka kwangu kisha nikae kimya? kama ni hivyo umepotea njia.


Kwa hiyo wewe unaacha kufanya kazi kwa vile mtu ulimpigia kampeni alishindwa? Kama huu ndio utendaji kazi wako basi inabidi ukae huko huko uliko maana huwezi joto la jikoni.


So far wewe ndio unaonekana mganga njaa na sidhani kama utetezi wako unahitajika hapa. Vyama vya upinzani vinashinda vijijini kila leo kama hukujua kuwa kigoma na tarime ni vijijini.

Hayo ya wewe kusubiria wenzako wafanye kazi ndio uje kuwaunga mkono ni uvivu usiofaa kabisa kwenye mapambano dhidi ya mafisadi wa ccm
 

Nani kafanya kazi nami nikamsubiria niende kumuunga mkono?
Lakini hata hivyo kama mtu kafanya kazi nzuri kuna kosa gani kuja kumuunga mkono?Kwahiyo kumuunga mkono kwa mfano slaa katika vita ya ufisadi baada ya kutoka na ile list of shame ni dhambi eehhh??
 

mhhh...

jiunge na wapiganaji na sio kuwataka wao kwenda vijijini on your behalf at the same time ukiwaita kuwa wao ni waganga njaa. Na kwa taarifa yako, kama ukileta umbea hapa dhidi ya wapinzani, ukumbuke kuwa sihitaji ruhusa ya yoyote yule kukujibu. Get it?
 

mimi siujuwi umbea najua facts tu kwa hiyo usihofu!
 

haya, gotcha mzee ! tutaonana mbele ya safari !
 
CHADEMA porojo nyingi na hakuna mkakati wowote wa utekelezaji.

Kila wakati ikija hoja hapa ya sera za CHADEMA utaona viongozi wao wanakuja kutoa thanks tu na hawajibu maswali ambayo wanapaswa kuyajibu.Badala yake wanakuja mashabiki kurefer watu kwa Ilani, Ilani gani unayorefer wana JF wakati viongozi wa CHADEMA wamekaririwa humu wakisema kuwa plan ya kuanzisha majimbo ni plan 0, wanatarajia mijadala izae plan 1 halafu sera kamili itoke baadae! sasa Ilani gani mnayowaambia watu wakasome???

Huu mjadala ni mojawapo tu ya mifano ya jinsi CHADEMA walivyo na porojo.
Nimeandika hapa mara nyingi na naendelea kurudia kuwa mchango wa baadhi ya viongozi wa CHADEMA katika kupiga vita ufisadi nchini unastahili kuheshimiwa na kupongezwa, ila CHADEMA kama chama hakiko tayari kuongoza taifa na sera yake kuu ya majimbo ni ndoto ya alinacha.
 

Maswali gani hayo ambayo bado hujayaweka hapa?


Je ni chama gani kiko tayari kuongoza nchi sasa hivi?
 

..........
 
Naona jinsi unavyoenjoy kutoka nje ya mjadala, hilo la chama mimi sitoligusa na wala simsukumi mtu kujibu swali langu.

Swali langu litajibiwa na watu wanatambua kuwa ni jukumu lao kujibu swali hilo ili kuuza sera za chama chao. Kama hawatafanya hivyo sitawasukuma kwa sababu mimi nimeuliza hilo swali kwa manufaa ya wana JF wote na si manufaa binafsi hivyo basi kuniadhibu kwa kutokujibu swali hilo hakuniathiri mimi tu bali pia chama kilichobuni hiyo sera na wana JF wengine wenye kutaka majibu.

kuhusu chama kinachoweza kuongoza nchi naomba nikuahidi kuwa sitaligusia kwenye thread hii.Thread yake inakuja.
 
Mjadala wa chama kinachoweza kuongoza nchi ni mkubwa.
I admit that I have "my answer" lakini siko tayari kwa debate.
 

wewe ndio inaonekana porojo zimekujaa kuliko hao chadema unaodai hapa kuwa wana porojo. Kama mtu unaweza kusema kuwa kuna chama hakiko tayari kuongoza nchi na bado ukawa huna alternative basi ujue kuwa umejaa porojo tu na hauko serious.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…