CHADEMA porojo nyingi na hakuna mkakati wowote wa utekelezaji.
Kila wakati ikija hoja hapa ya sera za CHADEMA utaona viongozi wao wanakuja kutoa thanks tu na hawajibu maswali ambayo wanapaswa kuyajibu.Badala yake wanakuja mashabiki kurefer watu kwa Ilani, Ilani gani unayorefer wana JF wakati viongozi wa CHADEMA wamekaririwa humu wakisema kuwa plan ya kuanzisha majimbo ni plan 0, wanatarajia mijadala izae plan 1 halafu sera kamili itoke baadae! sasa Ilani gani mnayowaambia watu wakasome???
Huu mjadala ni mojawapo tu ya mifano ya jinsi CHADEMA walivyo na porojo.
Nimeandika hapa mara nyingi na naendelea kurudia kuwa mchango wa baadhi ya viongozi wa CHADEMA katika kupiga vita ufisadi nchini unastahili kuheshimiwa na kupongezwa, ila CHADEMA kama chama hakiko tayari kuongoza taifa na sera yake kuu ya majimbo ni ndoto ya alinacha.