Mwafrika wa Kike
JF-Expert Member
- Jul 5, 2007
- 5,185
- 60
Unaona jinsi tunavyoenda nje ya topic? Hiki ndio ninachojitahidi kuepuka.
Unajua mtu ambaye sijaomba dhamana ya kuongoza nchi nikiwa na porojo ni tofauti sana na wale wanaoomba dhamana ya kuongoza nchi wakiwa na porojo. Hivyo basi usifananishe "porojo" zangu na za CHADEMA. Mimi najua kuwa sometimes huwa nina porojo na natambua kuwa sometimes porojo ni muhimu maishani, ila porojo katika mijadala ya msingi ya kuongoza nchi tusizikubali.
Kwa kuwa lengo la kwanza la CHADEMA wakiingia madarakani ni kuitisha mkutano wa Katiba sasa na kwa matazamo wangu nadhani kama hilo ni lengo wa kwanza basi CHADEMA haina sera kwa sasa. Kwa nini nasema hivyo, kwa mfano wananchi wakikataa mfumo wa majimbo kwenye katiba ni kivipi CHADEMA itatekeleza mfumo huo na kwa vile CHADEMA inaamini kuwa huo mfumo utatuletea maendeleo ya haraka sasa ni kivipi itatuletea maendeleo bila mfumo huo? Navyojua mimi sera za vyama vinatokana na katiba iliyopo. Kwenye sera ya utawala CHADEMA wamesema watapunguza mikoa kuwa 10 sasa kama katiba itakayoundwa itasema rais/chama hakitakuwa na mamlaka ya kugawa mikoa, je CHADEMA itakumia udikteta kuunda mikoa 10? Naomba muongozo.
Hoja hiyo hapo ya kujadili...
jibu swali mkulu mbona yengeyenge na longolongo kibao.... unahitaji maji ya kunywa?
Anzisha thread nitakujibu. Usipoanzisha basi mimi nitaanzisha muda ambao nilipanga kuanzisha. Thread hii amenzisha Sam akihitaji mwongozo wa CHADEMA.
Ukinipa maji nitashukuru.
Anzisha thread maana wewe ndio unadai kuwa na hoja. Mimi nakubali kuwa Chadema, CUF, TLP na wengine wanafaa na wako tayari kuongoza nchi na ccm ni wezi na mafisadi na hawafai kuongoza nchi. Kama unapinga hili basi anzisha thread na uwe tayari kujibu maswali yatakayoulizwa.
kwa sasa swali langu bado nauliza, kama chadema haiko tayari, ni chama gani kiko tayari?
Kama nilivyosema thread hiyo nilishapanga kuianzisha, muda wake ukifika nitaitundika. Tuvute subira.
Je na yale majibu ya sera za CHADEMA je?
Jibu swali nililouliza na ukitaka kuanzisha thread utaendeleza huko. Narudia tena swali langu. Kama chadema hawako tayari kuongoza nchi, je ni chama gani kiko tayari?
MWK una kawaida ya kushabikia vitu bila kupima halafu vinakukaba koo then unajaribu kuvitapika unagundua kuwa havitapikiki!!!
Hii ndio ilikufanya umtetee Mbowe kwa nguvu zako zote na kauli yake kuwa Balali kauliwa na serikali, halafu wewe mwenyewe unakuja kusema huamini kuwa Balali amekufa!
Unafanya tujiulize ulipokuwa unashabikia kuwa Mbowe anasema ukweli ulikuwa unatumia moyo au ubongo? Kwa hiyo mimi sitashangaa nikisoma unadenounce sera za majimbo, kwa sasa endeleo kuzishabikia kwa kutumia moyo mpaka pale utakapoanza kuushirikisha ubongo.
Jitihada zote unazofanya sasa hivi ni ili tubadilishe mjadala lakini fahamu kuwa kama mjadala utabadirika basi sio na mimi. Kwa mara ya mwisho narudia kuwa mjadala unaouingiza hapa unastahili thread yake ambayo nitaianzisha na wewe unaweza kuianzisha pia.
Kitu ambacho nina uhakika nacho kwa sasa ni kwamba hauna majibu anayohitaji Sam na wana JF wengine, hivyo basi endelea na mijadala mingine. Huu waachie wenye majibu yaliyoombwa.Sio lazima kila thread iwe na jina lako.
Kama leo ni siku ya mtihani na ili kufaulu ni lazima nijibu swali lako basi hesabu kuwa nimefeli mpaka wakati wa supplimentary exam ndio nitatoa jibu. Au utanidisco kwa hilo?
Kama hutaki kuuacha mjadala unayo haki ya kuendelea ila ukimbinyia Sam kupata jibu la swali lake unakuwa hujamtendea haki.
CHADEMA porojo nyingi na hakuna mkakati wowote wa utekelezaji.
Kila wakati ikija hoja hapa ya sera za CHADEMA utaona viongozi wao wanakuja kutoa thanks tu na hawajibu maswali ambayo wanapaswa kuyajibu.Badala yake wanakuja mashabiki kurefer watu kwa Ilani, Ilani gani unayorefer wana JF wakati viongozi wa CHADEMA wamekaririwa humu wakisema kuwa plan ya kuanzisha majimbo ni plan 0, wanatarajia mijadala izae plan 1 halafu sera kamili itoke baadae! sasa Ilani gani mnayowaambia watu wakasome???
Huu mjadala ni mojawapo tu ya mifano ya jinsi CHADEMA walivyo na porojo.
Nimeandika hapa mara nyingi na naendelea kurudia kuwa mchango wa baadhi ya viongozi wa CHADEMA katika kupiga vita ufisadi nchini unastahili kuheshimiwa na kupongezwa, ila CHADEMA kama chama hakiko tayari kuongoza taifa na sera yake kuu ya majimbo ni ndoto ya alinacha.
hoja hazijajibiwa naona watu wanajibizana
kiimarishwe chama makini kwa kupewa dhamana ya kushika usukani au la tutaipigia ccm mpaka utimilifu wa dahari
Basi usianze kulia bure....
MWK una kawaida ya kushabikia vitu bila kupima halafu vinakukaba koo then unajaribu kuvitapika unagundua kuwa havitapikiki!!!
Hii ndio ilikufanya umtetee Mbowe kwa nguvu zako zote na kauli yake kuwa Balali kauliwa na serikali, halafu wewe mwenyewe unakuja kusema huamini kuwa Balali amekufa! Unafanya tujiulize ulipokuwa unashabikia kuwa Mbowe anasema ukweli ulikuwa unatumia moyo au ubongo? Kwa hiyo mimi sitashangaa nikisoma unadenounce sera za majimbo, kwa sasa endeleo kuzishabikia kwa kutumia moyo mpaka pale utakapoanza kuushirikisha ubongo.
Jitihada zote unazofanya sasa hivi ni ili tubadilishe mjadala lakini fahamu kuwa kama mjadala utabadirika basi sio na mimi. Kwa mara ya mwisho narudia kuwa mjadala unaouingiza hapa unastahili thread yake ambayo nitaianzisha na wewe unaweza kuianzisha pia.
Kitu ambacho nina uhakika nacho kwa sasa ni kwamba hauna majibu anayohitaji Sam na wana JF wengine, hivyo basi endelea na mijadala mingine. Huu waachie wenye majibu yaliyoombwa.Sio lazima kila thread iwe na jina lako.