Asante kwa mchanganuo huu Mkuu.
Kama hutojali naomba kufahamu bei kwa mfuko mmoja!
Kingine Mkuu. Nimefatilia mjadala wenu (wewe na mdau mwanzisha thread hapo juu). Kwa ufupi sana, naweza sema nchini kwetu, kwa hali ilivyo sasa endapo hawataboresha mfumo wa utoaji elimu, inabidi elimu ya chuo kikuu angalau degree ya kwanza ndio iwe elimu ya msingi. Naomba kuishia hapa kwa sasa.
EEEeenHeeee!
Mkuu 'Heart Wood', sitaweza kukataa hayo uliyosema kuhusu elimu yetu, ingawa najua umetuunganisha sote humo. Hii ni aibu yetu sote, lakini lawama inajulikana inapostahil kuelekezwa. Siyo kwa sisi wahanga, bali hao wanaotulazimisha tuwe katika hali hiyo.
Wewe umeamua kusemea ubovu wa elimu yetu. Ninakubaliana nawe moja kwa moja; lakini nikuulize kama unaweza kunitajia ni eneo gani sasa unaloona hasa kuwa tuna nafuu juu yake kama taifa kwa ujumla. Nitajie tu eneo moja tunaloweza kujivunia kwamba sisi tunayo nafuu zaidi kuliko wenzetu katika mataifa yanayotuzunguka.
Baada ya kuyasema hayo ngoja nirudi kwenye habari yetu ya kuku..
Bei ya mfuko wa chakula cha kuku inategemea eneo ulipo wewe (umbali wa kinapopatikana chakula hicho toka kiwandani; na pia aina ya chakula chenyewe..
Kwa mfano, huwezi kutegemea kununua mfuko wa "Layer Starter" inayozalishwa Iringa kwa bei ile ile inayouzwa eneo lile, kama wewe unaishi na kufugia, kwa mfano Moshi au Mwanza.
Pili, bei ya mfuko wa "Layer Starter" ambao una protini nyingi ipo juu zaidi ya mfuko wa "Grower" na mfuko wa "Layer Complete" vile vile unayo bei tofauti.
Kwa hiyo mkuu wangu 'Heart Wood', nami ninakuomba ujitutumue kidgo kutafuta ni wapi utakuwa unanunua hicho chakula chako cha kuku na bei yake ni kiasi gani.
Moja ya jambo linalotuelemea sana siku hizi waTanzania ni hii tabia ya kutaka kuwa tegemezi sana, kutafutiwa ufumbuzi wa kila kitatizo kidogo bila kujihangaisha kidogo kujitafutia ufumbuzi huo.
Natumaini utakuwa umenielewa vizuri.
Nimetiririka tu hapa kwenye andiko hili, naomba kama kuna makosa ya kiuandishi uniwie radhi.