Usafiri wa train ni usafiri ninaoupenda sana...ni usafiri wenye risk ndogo na wa uwakika ukilinganisha na bus.
Kuhusu train via TAZARA zipo za aina mbili.
1. Train ya mizigo
2. Train ya abiria
~ Train ya abiria zipo za aina mbili
1* Express train...hii ni train ya route ndefu safari yake huanzia Zambia to Dar,sifa ya train hii Ina speed,inasimama vituo muhimu tu,inamuinekano mzuri kwa ndani,inabeba mizigo kwa limit, pia nauli yake imechangamka kidogo...
Ina madaraja matatu.
First....ni kachumba chenye vitanda vinne au viwili vya kukunja na kukunjua na meza moja..ni daraja lililo karibu na sehemu ya vinywaji na chakula, system charging na feni ipo na vyoo vyake vipo vzur sana.
Ni daraja lenye Bei ya juu kuliko class zote,ukipanda daraja hili hutojutia safari yako.
Second class..ni daraja la kati kuna seat ambazo zpo comfortable (super seat) na zpo seat zengne zinafanana tu na third class,kila behewa Lina system charging moja...kila behewa Lina feni 6,vyoo vyake vipo poa.
Bei yake ya kawaida tu,kama utapanda second class kata ticket ya super seat hutojutia safari yako.
Third class...halina tofauti sana na second class. Na Bei yake ndogo kulinganisha na first na second.
2* Ordinary train....hii train huanzia mbeya to Dar,ni train ambayo huchukua muda mrefu ktk safari zake,husimama kila ktuo ata porini as long as kuna huduma maalumu inahitaji kufanyika.
Nayo Ina class tatu, first.. second..na third.
Nauli yake hupishana elfu 2 adi elfu 5 na express.
Ukipanda ordinary sikushauri ata kidogo upande third class.