Naomba muongozo wako mkuu..p'se...!!

Naomba muongozo wako mkuu..p'se...!!

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906
Mke wa rafiki yangu anataka anipe dawa ya kuacha pombe nimuwekee mumewe yaani rafiki yangu kwenye pombe.ananibembeleza hadi imeshakua karaha.kisa akilewa anamsumbua na hatimizi malengo sababu ya pombe. Na huyo rafiki yangu ndo tunakunywa wote.sasa najiuliza, je huo si utakua usaliti?

2.mimi si ntakosa kampani ya bar?

3.akija kugundua mimi ndo nimempa dawa ya kuacha pombe wakati mimi bado nakunywa atajisikiaje?
mimi nipo njia panda.nifanyeje? mia
 
Kwanini huyo mwanamke asimpe mwenyewe..??

Na unauhakika gani ni dawa ya kuacha pombe??

Chunga sana kuwapa watu vitu kama hivyo.
Usije mpa mtu sumu ukaishia pabaya ..
ushauri wangu usijaribu..

Mwambie huyo dada ampikie mme wake
Chakula vizuri, amnunulie kama ndo bia
Au konyagi .. halafu afanye majongololo
Yake mwenyewe....
 
kuna dawa ya kuacha pombe zaidi ya rehab? au ndio kiuganga zaidi
 
mhh huyo mwanamke ana jini mahaba anataka akutie matatizoni.Halafu mbona anaonekana mganga mganga?dawa ya kuacha pombe kaitoa wapi?na wewe mpaka unakaa na huyo shemeji yako mkaanza kuongea haya mambo rafiki yako alikuwa wapi?maana haya ni mazungumzo mazito.Kuna walakini katika story yako
 
mpe afu na we mwenyewe jiwekee ka ya kufa mfe wote ka kuacha pombe muache wote
 
Hivi tangu lini dawa na pombe vikaambatana pamoja,kataa kabisa
 
Kwanini huyo mwanamke asimpe mwenyewe..??

Na unauhakika gani ni dawa ya kuacha pombe??

Chunga sana kuwapa watu vitu kama hivyo.
Usije mpa mtu sumu ukaishia pabaya ..
ushauri wangu usijaribu..

Mwambie huyo dada ampikie mme wake
Chakula vizuri, amnunulie kama ndo bia
Au konyagi .. halafu afanye majongololo
Yake mwenyewe....

usipofwata huu ushauri basi,huna bahati ila chunga sana,mmepata wapi mda wa kuongea na mkke wa mweinzio namna hii halafu ashindwe hata sekunde ya kumwekea hiyo miti shamba yake mwenyewe?take bro,jf stil need you
 
Mmmh huyo mwanamke ana mbwembwe,acha amuwekee mwenyewe..usithubu2 kushirikiana nae.
 
Back
Top Bottom