Naomba mwongozo: Nina Suzuki Carry, nataka kumpa Dereva ambaye atakuwa akiniletea malipo kwa wiki

Mzalendo_Mkweli

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2012
Posts
2,025
Reaction score
1,270
WanaJF habari,

Nina Suzuki Carry nataka kumpa Dereva ambaye atakuwa akiniletea malipo kila baada ya wiki moja.Mimi si mzoefu sana katika biashara hii hivyo nimejaribu kuwauliza watu mbalimbali ili niweze kupata picha jinsi mkataba husika utakavyo kuwa. Katika mchakako huu wa kupata mwongozo nilichoambulia cha maana ni malipo i.e yawe kati ya shilingi 120,000 na shilingi 130,000 kwa wiki ILA mambo mengi sijapata mwanga mfano:-


  1. Nani atakayekuwa akiweka mafuta
  2. Minor & Major maintenance nani atahusika
  3. Zile regular Service (baada km 3000) nani atahusika
  4. Ikitokea gari kukamatwa na Trafic nani atalipa faini

Waheshimiwa mlio na uzoefu nawaombeni mnitoe ujinga kidogo ili mkataba utaoandaliwa na mwanasheria uwe sahihi. Natanguliza shukrani.. Ahsante
 
1. Mafuta ya mwanzo unaweka wewe, halafu kila siku akiirudisha yawe kama ulivyompa.

2. Minor and major maintannance ni wewe mwenye mali unless iwe mmekubalina kila kitiu juu yake na bei ya kukupa kwa siku inapunguwa.

3. Kama namba mbili.

4. Faini ni driver mwenyewe kwani wewe unampa kila kitu kiko safi utunzaji na uendeshaji inabidi ni yeye achunge. Unless karipoti ubovu ukamwambia tembea hivyo hivyo.

Yote hayo ainisha wazi kwenye mkataba.

Kumbuka; Kama una ugonjwa wa moyo usifanye hiyo kazi. Kama hauna ugonjwa moyo jitayarishe unless dereva awe kashushwa na uzi wa bubui kutoka mbinguni tena si Mtanzania.

Angalizo; ni biashara nzuri ikiwa utaanza na carry tatu kwa mara moja na si moja, mafanikio ya moja pekee ni ya muda mrefu na itategemea na bahati na si ujuzi.
 
Je hayo malipo ya Tshs 130,00 kwa wiki unayaonaje?

Je ni busara kuwa unabadili dereva kila baada a muda gani?

Ahsante


 
Je hayo malipo ya Tshs 130,00 kwa wiki unayaonaje?

Je ni busara kuwa unabadili dereva kila baada a muda gani?

Ahsante

Si vyema kubadili dereva kama uliyenae ni mzuri na anafaa.

Kuhusu malipo siwezi kuingilia, kuna anaeridhika na chini ya hizo na kuna anae demand juu ya hizo. Inategemea na mkataba wenu.
 

Kama mama faizafox alivyosema ni sawa kabisa
Nataka kusisitiza hii biashara ni ngumu kuliko unavyofikiria, Mzee wangu alifanikiwa tu mimi nikiwa nasimamia mwenyewe(kondakta) ninapokua zile likizo ndeeeefu za vyuoni zaidi ya hapo no. Ni vigumu sana almost impossible kupata driver mzuri atakae ijali gari na kuleta hesabu kama inavyotakiwa.
Kitu kingine lazima ujue Suzuki carry ni gari ndogo sana kilo350 tu yenye bodi ya kubeba mzigo mkubwa hivyo zinakufa mapema.
Ila ndo mazingira ya biashara za kibongo ni kupambana tu.
 

Hongera kwa Kumiliki Japo Carry. Mimi sina ushauri ila nafikiri tunaweza kufanya biashara. Mimi natafuta Suzuki Carry ya kukodi, yaani, naingia mkataba na mwenye carry, tunaandikishana mpaka serikali za mitaa. Kisha hiyo carry inakuwa mkononi mwangu (japokuwa inaendelea kuwa mali yako) na tunakubaliana kiasi cha pesa nitakachokuwa nakupatia kila mwezi.
Kuhusu gharama ulizozitaja hapo juu; Gharama zote nazibeba mimi isipokuwa zile kubwa kubwa (major maintence services kama ulivyoziita). Jukumu lako wewe ni kulikagua gari yako pale unapoona inafaa coz ni mali yako.
Tuwasiliane kwa 0685624339 ama barua pepe: kasanga21@gmail.com. Nipo Dar ndugu yangu.
 

Mimi sina ushauri kwa haya unayoulizia. Ila nakuletea business proposal ukiikubali tufanye kazi.

Mimi ni Mfugaji wa ng'ombe wa maziwa, ninahitaji usafiri wa kubebea majani ya ng'ombe na mashudu. Kama utaafiki tuingie mkataba, nakupatia kwa wiki hiyo 130,000/-. Ujira wa dereva juu yangu, maintenance juu yangu, mafuta juu yangu.
 

Wazo zuri sana hili pia.Ila kwa mkataba wa namna hii no bora malipo yawe ya mwezi.Maana Carry nyingi zinafanya kazi mazingira ya mjini na pembezoni kwake ambapo ni salama zaidi.
Kuna mashamba mengi ya nje ya mji sana njia mbovu ni miezi sita tu huna gari.
 
Mleta mada hii biashara ni nzuri.
Na unaweza ukaanza na hata hiyo moja,ili ujue changamoto zake.
Mie namshukuru mungu nilijiandaa kiachangamoto haikuwa sana shida kwangu.
Kesi kubwa za gari hizi ni kufa shock up,ikikosa kufa basi spring yake inakufa.Shock pari inafika hadi laki tatu,sasa kama unapesa za mawazo ukistukizwa gharama hizo lazima uone biashara ngum.

Muhim ni kuwa na nidham ya pesa,na hesabu sio 130,000 ni 120,000 ndio bei za siku hizi.Ukibana sana ndio unaukaribisha umarehem wa gari yako.
Hakikisha wewe ndio unaulizia matataizo ya gari yako na sio usubiri dereva ndio akuambie.Madereva wengi sana wanapenda mabaso wanaofuatilia gari zao.Nie Experience mie kweny gari zangu.
Kesi nyingi ukiwasikia madereva wakilalamika ni kwamba mabosi wao wanaangalie hela tu,lakini ukiamuambia tatizo la gari kila siku yeye hana hela na ikifika hesabu hataki upungue,na kama ikitokea siku akatengeneza kitu kwenye gari basi atasema kila siku katengeneza gari nzima.
Mfano mie ninao ndani ya nyumba yetu,Sister wangu anavyo viwili lakini kila siku lazima nicheke yeye na madereva wake wanavyozinguana.Cha kushangaza dereva wako mmoja ndio alisimamia Gari yangu ya mwanzo na tunaendanae vizuri ile mbaya.Mpaka amenipa hamasa ya kuongeza na yeye kuwa dereva msimamizi na hesabu zote zinatoka kwake na anasimami kesi zote za matengenezo.Muhim pia ni kujenga imani na kuona makusudio na dhamira yako inatimia.
Hakuna biashara isiyo na changamoto na hakuna biashara nyepesi.Penda sana kumjali dereva wako na familia yake.
Kuna watu hawajui kuumwa wala msiba,wao kila siku wanataka pesa.Mie huwa sioni hii kesi ya kila mwenye gari kusisitiza upate dereva muaminifu,wakati wewe Tajiri mwenyewe kimeo.We onyesha uungwana kwa mfanyakazi wako kama ndugu basi na yeye atajadili kazi yake kama ndugu.

Ni hayo tu.
 

Mkuu asante kwa ushauri unaoeleweka, naomba kama una mkataba wa kupeana na dereva katika biashara hii fanya msaada wa attachment ya mkataba na kama pia kunamtu yoyote mwenye mkataba wa biashara kama hii msaada apo wa mkataba please
 
Nimeona pia utaratibu wa mkataba wa miaka2,yaani miezi 24~utaratibu ni kuwa baada ya miaka2 gari ni la driver~kila wiki anakuletea 175,000/= so kwa mwezi ni laki7(700,000/=) kwa mwaka ni 8,400,000/= kwa miaka 2 inakuwa 16.8m
Utaratibu huu ni kuwa driva anakuwa mwangalifu sana na gari kwani indirectly chombo~gari ni yake
Mafuta na matengenezo madogo madogo ni juu yake
Kuna jamaa yangu ana hizi carry 3 utapenda anavo~sanya cash mwisho wa wiki laki 5.25 (525,0000/=)
Biashara haina usumbufu kabisa~ila angalizo Mungu asaidie upate driver mzuri anayejua mkataba ni nini
Nawasilisha viongozi
 
Nimekaagiza kamoja kanakuja mwezi ujao ila saizi vimepanda sana bei. Ngoja nami nije nione changamoto zake. Ila mpaka hapo nimeanza kuona kilicho mbele yangu.
 
Ninayo carry moja nimempa driver wiki ya pili sasa. Ikiwa mambo yatakwenda vizuri nitaagiza mbili nyngine.
 
Ka kwetu kameanguka juzi tu. Kalifanya kazi mwezi mmoja. Garage wanataka laki 8 kunyoosha.

Ni sheedah.
 
Hizi Carry bei yake imefika ngapi kama nataka kununua hapa Tz?
 

Uchambuzi wako uko safi ila angalizo lako si la kweli,kuna jamaa namjua ameendesha carry miezi 6 sahv amenunua nyingine au mda mrefu kwako ni upi
 
Uchambuzi wako uko safi ila angalizo lako si la kweli,kuna jamaa namjua ameendesha carry miezi 6 sahv amenunua nyingine au mda mrefu kwako ni upi

Kumbuka kuendesha mwenyewe au anaeendesha kama dereva ni tofauti na mwenye mali anaempa dereva anaeendesha.
 
Hapa Bongo kwenye Yard vinauzwaje?
Ukiagiza toka Japan mpaka kutoa bandarini inagharimu kiasi gani?
Used inayofaa kutoka kwa mtu inahitaji kama kiasi gani? Unywaji wake wa mafuta vipi?
Nataka kutafuta kamoja chap kwa issue zangu za mifugo na kilimo, inaonekana tuna save sana mafuta.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…