Naomba mwongozo: Nina Suzuki Carry, nataka kumpa Dereva ambaye atakuwa akiniletea malipo kwa wiki



Mara ya mwisho kuagiza carry Japan ilikwa mwaka 2012. Ilinighaimu kama $1100 kila moja na zilikuwa sita ndani ya container.Final destination ni Znzbar.
 
Kumbuka; Kama una ugonjwa wa moyo usifanye hiyo kazi. Kama hauna ugonjwa moyo jitayarishe

Angalizo; ni biashara nzuri ikiwa utaanza na carry tatu kwa mara moja na si moja
Kwa nini ni biashara nzuri kama inabidi ujiandae kupata pressure? Uwezo mdogo wa kujieleza wa Watanzania.
 
Mara ya mwisho kuagiza carry Japan ilikwa mwaka 2012. Ilinighaimu kama $1100 kila moja na zilikuwa sita ndani ya container.Final destination ni Znzbar.
Mkuu km carry moja ipo pending tuingie mkataba
 
Aha utaratibu huu ni mzuri , kwa yeyote mwenye carry, mimi ni dereva nina "VALID LICENCE" nahitaji kukodi Nipo Dar 0759601820
 
Kwanza naomba nikushukuru kwa kunipa wazo ambalo sikulifikiria kabisa.Sasa naomba niulize maswali machache:-

1. Katika scenario uliotoa, nani atakuwa analipa Insurance, Income tax, road Licence?
2. Zile Service za kila baada ya km 3000, nani atakuwa analipia hizo gharama?

Pia naomba kukuliza kama unajua kuhusu hili suala la kulipa Income Tax TRA kwa hizi Suzuki carry. Mimi kwa sasa nalipia Income Tax gari mojamoja Tsh. 318000 kwa mwaka, ila nisikia kwa mtu (Sina uthibitisho) kwamba naweza kulipia magari yote kwa pamoja ambapo nitatozwa bei pungufu.

Nawakilisha.

Ahsante


 
Kwanza napenda kukushauri ni vyema ukaagiza kuliko kununua hapa. Kama Shilingi yetu ikiimarika bei za haya magari si kubwa, nimeagiza gari moja ambayo naitoa bandarini wiki hii ambayo imenigharimu kama Tshs 8,200,000 (gari kufika nyumbani kwangu). Hapo nitabakiwa na Insurance pamoja na malipo ya kuanzia ya Income Tax.

Ahsante

Hizi Carry bei yake imefika ngapi kama nataka kununua hapa Tz?
 
Wazee tunashukuru sana kwa kuoneshana fursa kwenye upande huu.. Mbarikiwe sana
 
Hakuna biashara isiyo na changamoto wapendwa.Nachoona biahsra yoyote ile kinachotakiwa ni uvumilivu tu na kuwajibika tu ndo utaona mafanikio,,Na idea nyingi kwnye hili jukwaa ni nzuri kweli ila pia ingekua vizuri tukawa tunaleta mrejesho mtu ajue na changamoto zake asije kata tamaa kabla
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…