Mkuu kwanza kwa pikipiki maarufu hapa bongo nazungumzia Tvs na Boxer hizi huwezi kununua india moja kwa moja sababu tayari kuna dealer ambaye ni CAR GENERAL Tz ltd huyu anauza Tvs bike na Tvs king yani kama unataka mzigo unanunua kwake then wewe ndio unauza kwa mtu wa mwisho. Bei zao kwa jumla bajaji wanauza 7.1M na Tvs bike wanauza 2.2M lakini sasa hizi inategemea kuna 150 na 125 cc bei zinatofautiana. Vigezo na masharti yao wacheki hapo Posta azikiwe ukishuka tu stendi ya daladala.
Kuhusu Boxer ni Mo ndio anasimamia show kwa hapa Bongo wote wananunua kwake. Tembelea ofisi zao zipo K.koo gerezan nafikiri. Mengine watakwambia wenyewe ofisini.
Ila kama una mtaji mkubwa ni biashara nzuri sababu kuna kipindi ziliisha kwa agents wengi hapa dar watu wakawa wananunua kwa dau kubwa zaidi kutoka kwa agents wa mikoani.
Hapo kwa Tvsking (Bajaji) soko ndio kubwa zaidi kwani watu wengi hulipia mzigo kabla hujafika bandarini ukifika wewe unasambaza tu na kuleta mwingine. Nimemaliza