Naomba nijibiwe swali langu. Mtaala mpya wa elimu somo la dini

Asiye na dini hatafanya chochote

Somo na dini haliongezi credit kwa hiyo ufanye au usifanye ni sawa tu.

Dini ni ya mtu na Mungu wake sio mitihani yetu
 
Sio hilo tu unafiki wa hawa viongoz mbumbumbu na wenye roho mbaya ni kuendelea kufanya kiswahili kitumike shule za msingi wakat watoto wao wanasona english medium,haya maviongozi yana roho mbaya sana
Tatizo la kiswahili siyo la msingi sana maana secondary tunatumia kingereza ila wanafunzi bado awaelewi masomo ....tatizo ni mfumo wa ufundishaji masomo katika shule za serikali....maana hata ilo somo la kiswahili wanafunzi wana feli ....somo la kingereza lipo toka primary ila wanafunzi wanamaliza miaka 7 bila ya kujua kingereza na secondary wanasoma masomo kwa kingereza na somo la English lipo wanasoma miaka 4 ila wanamaliza awajui kingereza ....tatizo ni ufundishaji siyo lugha.
 
Msingi wa Lugha lazima uanze utotoni sio utu uzima mkuu,hivyo basi lazima English ianzie shule za awali kama Lugha ya kufundishia na Kiswahili kiwe somo ,tuache siasa English ni Lugha ya dunia na maarifa.
 
Msingi wa Lugha lazima uanze utotoni sio utu uzima mkuu,hivyo basi lazima English ianzie shule za awali kama Lugha ya kufundishia na Kiswahili kiwe somo ,tuache siasa English ni Lugha ya dunia na maarifa.
Hayo unayosema hayawezi kuwa na tija kwa sababu mitaani tunatumia kiswahili ....mwanafunzi kushindwa hesabu primary ni ufundishaji siyo lugha ...lengo la kwenda shule siyo kujua lugha ya kingereza tu ...shule za serikali hata zikitumia English kuanzia primary haziwezi kufanya vizuri ...huo ndiyo ukweli
 
Vichwa maji bhana utawajua tu,wengi wenu mnajificha nyuma ya keyboard kukataa Islamic knowledge eti kisa chuki zenu dhidi ya uislamu!
Kwani haikuepo mwanzo?
 
Naomba kuuliza, je hii italazimu shule za kiislam kufundisha biblia na wanafunzi wakristo kutovaa mavazi ya kiislam , kadhalika shule za kikristo kufundisha Quran na wanafunzi wa kiislam kuvaa mavazi Yao husika?
 
Mara nyingi Wanafunzi wasiokuwa na dini au wasiopenda kwenda kwenye vipindi vya dini hupata usumbufu sana wakati wa vipindi vya dini. Wanakuwa harassed au kulazimishwa kuhudhuria dini.
 
Haya yatakuwa matumizi mabaya ya pesa za walipakodi
Mzee masheikh wanatafutiwa kazi Angalau na wao wafundishe mashuleni sio misikitini..

Si unajua pesa ndogo madrasa sasa hivi watakula pesa ya kutosha kila mwezi Naamini watafurahi sana..Maalimu
 
Nimecheka kusoma kipengele kinachodai hao walimu wa dini ya kiislamu sharti waajiliwe na serikali.
Yaani serikali hii inayoshindwa kuajiri walimu wa masomo ya sayansi leo inatakiwa iajiri walimu wa dini. Ngoja tuone haya maajabu ya Mkenda.
Ya kweli hayo?
 
Mambo ya ajabu sana, itahitaji utashi mkubwa wa kisiasa na uongozi jasiri sana kukomesha kasumba hii.
 
Asiye na dini hatafanya chochote

Somo na dini haliongezi credit kwa hiyo ufanye au usifanye ni sawa tu.

Dini ni ya mtu na Mungu wake sio mitihani yetu
Shule nyingi walimu, viranja na wanafunzi wafia dini huwa wanawalazimisha wanafunzi kuingia katika vipindi vya dini.
 
Shule nyingi walimu, viranja na wanafunzi wafia dini huwa wanawalazimisha wanafunzi kuingia katika vipindi vya dini.
Ni kweli kabisa mimi yalinikuta
 
Kweli kabisa, pia wameunda chombo chao mbadala wa TIE nayo wanataka ilipwe na serikali.
Hii ni hatari,labda kama serikali itafanya kuwatambua walimu iliowaajiri yenyewe ambao ni waumini wa hizo dini. Lkn kusema hizi taasisi za dini ndio ziwaajiri na serikali ilipe,hapo siyo sawa.
 
Hii ni hatari,labda kama serikali itafanya kuwatambua walimu iliowaajiri yenyewe ambao ni waumini wa hizo dini. Lkn kusema hizi taasisi za dini ndio ziwaajiri na serikali ilipe,hapo siyo sawa.
Wajanja, walianza kuitaka serikali kuanzisha combination zenye somo la Isamic na Arabic language. Serikali ilipoanzisha kwenye mashule yake ikaacha liwe jukumu la wakuu wa shule zilizoanIsha kupanga walimu kama ilivyoada.
Walivyoona hiyo habari ya serikali kuwatambua walimu wa kiislam ili wafundishe waliiogomea hadi kupelekea waziri akaombe maoni ya mufti. Mufti kashirikiana na mwenzake wa Zanzibar na wale wanaoendesha MMU wakaja na hayo mapendekezo, ya mtaala, vitabu, taasisi ya elimu ya kiislam na kuagiza serikali iwalipe hao walimu wataopendekezwa na taasisi hiyo. Ndo tunasubiri tuone uprofesa wa Mkenda.
 

Wapuuzi wanaturudisha nyuma na upuuzi wa dini,sehemu za umma kuleta dini ni upuuzi mtupu.
 
Wapuuzi wanaturudisha nyuma na upuuzi wa dini,sehemu za umma kuleta dini ni upuuzi mtupu.
Kuna mambo ya chini chini walifanya jitihada kuingiza hayo mambo kwenye majeshi ila walikataliwa ila jitihada za kuingiza majeshini hijabu zipo mbioni ...walitaka kuanzia JKT wakadai watoto wa kike jkt wajisitili kwa kuvaa hijabu kwenye polisi nako wameingia ka kuwalazimisha vazi la suruali badala ya sketi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…