Naomba nipatiwe elimu kuhusu umaliziaji wa kujenga nyumba juu (Gypsum Board na PVC Board)

Naomba nipatiwe elimu kuhusu umaliziaji wa kujenga nyumba juu (Gypsum Board na PVC Board)

Umemshauri vizuri naongeza nyama kidogo. Kwa sehemu ya nje kwenye fascia boards kwa chini huwa ndipo PVC hutumiwa. Gypsum boards kwa nje hazifai kutokana na unyevu na maji ya mvua. So atatumia zote pvc na gypsum, pvc kwa nje na gypsum kwa ndani.

Bei za PVC zikoje wakuu?
 
Nakushauri tu chukua yoyote yenye gharama nafuu, usitoboe mfuko sana kwenye hiyo sehemu ya gypsum maana iwe brand yoyote ikivujiwa na maji ni lazima eneo lililovujiwa ulibadilishe

Gypsum ni majina tu lakini ukifunga kama haijapata bughudha inaishi sana. Mie nimejenga nyumba kadhaa za wapangaji mwanzo nilikuwa naweka ANDIKA ila baadae nikawa naweka za bei nafuu ila zote zina mwonekano sawa na hazijawahi kusumbua. Hapo mchawi kuvujiwa tu
Nashukuru mkuu nalifanyia kazi
 
Nakushauri utumie gypsum board instead of pvc (kwa dsm) pvc zinasharabu joto zaidi na kama nyumba yako fupi haina ac utajuta!
Board azitofautiani sana ila kuna za thailand (most expensive) na za tz! Kuna standard, bbg, andika, double elephant etc.
Hapo bbg ndio cheap zaid ila skushauri utumie kwa kuwa ni laini zaid ukiztoa 100 kkoo site zitafika nzima 90 na kwnye kuzikata znakatika vibya! Tumia double elephant kwa kkoo now znauzwa 15-16k
Nashukuru mkuu kwa ushauri na ushuhuda wako
 
Umemshauri vizuri naongeza nyama kidogo. Kwa sehemu ya nje kwenye fascia boards kwa chini huwa ndipo PVC hutumiwa. Gypsum boards kwa nje hazifai kutokana na unyevu na maji ya mvua. So atatumia zote pvc na gypsum, pvc kwa nje na gypsum kwa ndani.
Barikiwa mkuu
 
Ina maana mtaani kwako hakuna mafundi? Au ulipenda tu kuja kutuzodoa hapa jukwaani kwamba nawe una ka kibanda? Tuheshimiane bro![emoji16][emoji16]
Mkuu siyo hivyo kama umenielewa tofauti nisamehe
 
Amen mkuu, tunasubiri mrejesho wa namna utakavyo implement ili na wengine wajifunze Mhakiki
 
Wakuu nisiwachoshe naomba nijikite kwenye mada.

Nina kibanda changu Cha vyumba vinne kimoji ni self, public toilet, sebule, dinning, jiko na stoo na Niko kwenye hatua ya finishing.

Naomba nipate Elimu kuhusu gypsum board aina zake, wazalishaji na ubora wake pamoja na bei zake za mjini(DSM).

Pia, naomba nipate Elimu kuhusu pvc board gharama zake zikoje kwa bei ya mjini DSM na wazalishaji wake na ubora wao.

Kuna tofauti Gani za ubora wa hizi materials tajwa hapo juu na udhaifu wake hasa kwa kuzilinganisha.

Natanguliza shukrani.
sio nyumba ya juu ni hatua ya Dari mkuu
 
PVC BOARD ni bora mara mia kama nyumba yako inavuja,lakin usipige Gpsum board kwenye nyumba inayovuja UTAJUTA🙏🙏
 
Back
Top Bottom