Naomba nitumie nafasi hii kuwataka radhi ndugu zangu. Nimetukanwa leo nikashukuru tu

Naomba nitumie nafasi hii kuwataka radhi ndugu zangu. Nimetukanwa leo nikashukuru tu

Bill Lugano

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
1,189
Reaction score
6,450
Napenda niwape kwanza salamu toka kwa Mark Twain Gerald jamaa yangu toka Finland. Nilikuwa huko nmerudi siku chache zilizopita. Huwa anapenda kuingia ingia JF asome threads za English acheke sana, anasema anawapenda.

Nmerudi na kukuta Dar Ukiwa nje ya Ofisi na Nje ya Gari au Home kuna joto.najikuta kila wakati nalazimika niwe home nitumie AC,kwenye Gari ni Full Time AC. Sikumbuki kama kuna gari yangu hata moja ambayo nmewahi zima AC. Ziwe zile Range mbili,Merc,BMW,Ford Ranger au GMC.

Leo nlikuwa na Mercedes Benz.mara nyingi jumatatu napenda tumia Benz.nikawa nmetoka kwenda pata lunch hotelini katikati ya jiji. Basi nikapark gari nkaenda kuangalia ustaarabu wa chakula.

Baada ya muda nkatoka ili niondoke nikakuta kuna mtu ameni block. nyuma ya gari yangu kapark Toyota IST. Mlinzi akanambia mwenye gari kaingia ndani.kuna meza amekaa akaenda akanionesha kuwa amekaa meza ilee.

Maskini ,very innocently nikaenda hiyo meza nikakuta kijana mmoja mnene na mdada wamekaa.nikawasilimia na kumwambia yule dada "samahani sista umepark IST nyuma ya Gari yangu"

Eti jamani hapo nlikosea nini ndugu zanguni? Yule dada akashtuka kidogo huku amekunja uso. " Mi sijaja na IST samahani kaka gari yangu ni Harrier" sikufahamu kwa nini alikunja sura.

Basi nikarudi kwa mlinzi kumwuliza mbona yule dada amekataa kuwa si yeye mwenye IST?Ndo mlinzi kunambia ni yule Bonge ndo mwenye IST. Basi nikajisikia unyonge sana.

Nikaenda mwambia yule Jamaa kuwa amepark IST yake nyuma ya Gari Yangu akanambia gari gani huku kakunja sura.ndo nikamwambia ni Mercedes Benz Rangi ya Silver namba D** akanijibu kwa hasira kidogo
"basi wala hauna haja ya kutoa maelezo mengi"

akatoka huku anatukana kuwa "watu wengine mna mambo ya kijinga sana"

Sikuelewa why aseme hivyo. Nlimwambia tu sorry kama nmekukwaza ila hukufanya ustaarabu kupark IST nyuma ya GARI kama ngerudi nyuma bila kuangalia si ungepata hasara ya IST yako kuharibika?

nmejikia vibaya why kitu kidogo tu apaniki namna ile.nlimtaka radhi kuwa asijisikie vibaya.mimi naelewa haiwezekani wote tukaendesha gari za Wazungu. Ukipata Toyota,Nissan,Subaru n.k ni hatua pia wala si suala la kujisikia mnyonge.angalau una usafiri ukijipanga unatafuta gari hata kwa mil 50. Si unaweza pata gari nzuri tu?

nawaombeni radhi kama huwa mnakwazika naposema mimi vyombo vya usafiri vya kijapani huwa siviamini sana labda yale ma V8.sisemi kwa ubaya mbona mtu akisema hapendi gari za ulaya na marekani mi sichukii?si kila mtu anapenda anachopenda?hamna haja ya kuchukiana. Na kuanzia leo naondoa ile dhana kuwa IST ni gari za wadada walioko Chuo au Sekondari.naicha hiyo.
 
Back
Top Bottom