MIXOLOGIST
JF-Expert Member
- Mar 1, 2016
- 14,311
- 36,056
Wasalaam wana JF
Kwa wale wanaoamini uzima wa milele yaani maisha baada ya kufa yenye raha (mbinguni) na yale yenye mateso (motoni)
Ni hivi, kigezo ni kimoja tu matendo yetu, kwa urahisi wa rejea tusome:
Ufunuo 20:13
Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake.Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.
Mathayo 25: 31-40
Hukumu ya mwisho
31“Wakati Mwana wa Mtu atakapokuja katika utukufu wake na malaika wote wakiwa pamoja naye, hapo ataketi juu ya kiti chake cha enzi kitukufu.
32Mataifa yote yatakusanyika mbele yake, naye atawatenganisha watu kama mchungaji anavyotenganisha kondoo na mbuzi.
33Atawaweka kondoo upande wake wa kulia na mbuzi upande wake wa kushoto.
34“Kisha Mfalme atawaambia wale walio upande wake wa kulia, ‘Njoni enyi mliobarikiwa na Baba yangu; pokeeni ufalme mliotayarishiwa tangu kuumbwa kwa ulimwengu.
35 Maana nilikuwa na njaa nanyi mkanipa chakula; nilikuwa na kiu nanyi mkanipa maji; nilikuwa mgeni nanyi mkanikaribisha;
36 nilikuwa uchi, mkanivika; nilikuwa mgonjwa nanyi mkaja kunitazama; nilikuwa gerezani nanyi mkaja kunitembelea.’
37 Hapo, hao watu wema watamjibu mfalme ‘Bwana, ni lini tulikuona mwenye njaa nasi tukakupa chakula, au ukiwa na kiu nasi tukakunywesha maji?
38 Ni lini tulikuona ukiwa mgeni nasi tukakukaribisha, au bila nguo nasi tukakuvika? 39Ni lini tulikuona ukiwa mgonjwa au mfungwa nasi tukaja kukutazama?’
40 Mfalme atawajibu, ‘Kweli nawaambieni, kila kitu mlichomtendea mmojawapo wa hawa ndugu zangu wadogo, mlinitendea mimi.’
Sasa basi ni nini cha kufanya:
1. Tufanye matendo mema;
2. Tuache matendo mabaya;
3. Kama tumesahau kabisa, tusitende dhambi
Matendo mema ni yapi:
2. naye akaanza kuwafundisha:
4. Heri walio na huzuni,maana watafarijiwa.
5. Heri walio wapole,maana watairithi nchi.
6. Heri wenye njaa na kiu ya kufanya atakavyo Mungu,maana watashibishwa.
7. Heri walio na huruma,maana watahurumiwa.
8. Heri wenye moyo safi,maana watamwona Mungu.
9. Heri wenye kuleta amani,maana wataitwa watoto wa Mungu.
10. Heri wanaoteswa kwa sababu ya kufanya atakavyo Mungu,maana ufalme wa mbinguni ni wao.
11. “Heri yenu nyinyi watu wakiwatukana, wakiwadhulumu na kuwasingizia kila aina ya uovu kwa ajili yangu.
12. Furahini na kushangilia maana tuzo lenu ni kubwa mbinguni. Hivyo ndivyo walivyowadhulumu manabii waliokuwako kabla yenu.
14. “Nyinyi ni mwanga wa ulimwengu! Mji uliojengwa juu ya mlima hauwezi kufichika.
15. Wala watu hawawashi taa na kuifunika kwa debe, ila huiweka juu ya kinara ili iwaangazie wote waliomo nyumbani.
16. Vivyo hivyo, ni lazima mwanga wenu uangaze mbele ya watu, ili wayaone matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.
18. Kweli nawaambieni, mpaka hapo mbingu na dunia zitakapopita, hakuna hata nukta moja au sehemu ndogo kabisa ya sheria itakayoondolewa, mpaka yote yametimia.
19. Basi, yeyote atakayevunja hata amri moja ndogo kuliko zote, na kuwafundisha wengine wafanye hivyo, huyo atakuwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni. Lakini yule atakayezishika na kuwafundisha wengine, huyo atakuwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni.
20. Ndio maana nawaambieni, wema wenu usipozidi ule wa waalimu wa sheria na wa Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.
37 Yesu akamjibu, “Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote na kwa akili zako zote.’ 38 Hii ndio amri kuu, tena ni ya kwanza. 39 Na ya pili inafanana nayo, nayo ni hii: ‘Mpende jirani yako kama nafsi yako.’ 40 Amri hizi mbili ndio msingi wa sheria zote na Maandiko ya manabii.”
TUEPUKE NINI
1. Unafki;
2. Kuna wale wenzangu na mimi ambao tunashinda kwenye majumba ya ibada na kufanya sala ndefu ila tukitoka huko tunafanyia wenzetu ubaya, tunakumbushwa kwamba, sala siyo kipimo cha kuamua wapi tutaenda, ni matendo yetu ; and
3. Tusihukumu wengine
Tafakari chukua hatua.
Kwa wale wanaoamini uzima wa milele yaani maisha baada ya kufa yenye raha (mbinguni) na yale yenye mateso (motoni)
Ni hivi, kigezo ni kimoja tu matendo yetu, kwa urahisi wa rejea tusome:
Ufunuo 20:13
Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake.Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.
Mathayo 25: 31-40
Hukumu ya mwisho
31“Wakati Mwana wa Mtu atakapokuja katika utukufu wake na malaika wote wakiwa pamoja naye, hapo ataketi juu ya kiti chake cha enzi kitukufu.
32Mataifa yote yatakusanyika mbele yake, naye atawatenganisha watu kama mchungaji anavyotenganisha kondoo na mbuzi.
33Atawaweka kondoo upande wake wa kulia na mbuzi upande wake wa kushoto.
34“Kisha Mfalme atawaambia wale walio upande wake wa kulia, ‘Njoni enyi mliobarikiwa na Baba yangu; pokeeni ufalme mliotayarishiwa tangu kuumbwa kwa ulimwengu.
35 Maana nilikuwa na njaa nanyi mkanipa chakula; nilikuwa na kiu nanyi mkanipa maji; nilikuwa mgeni nanyi mkanikaribisha;
36 nilikuwa uchi, mkanivika; nilikuwa mgonjwa nanyi mkaja kunitazama; nilikuwa gerezani nanyi mkaja kunitembelea.’
37 Hapo, hao watu wema watamjibu mfalme ‘Bwana, ni lini tulikuona mwenye njaa nasi tukakupa chakula, au ukiwa na kiu nasi tukakunywesha maji?
38 Ni lini tulikuona ukiwa mgeni nasi tukakukaribisha, au bila nguo nasi tukakuvika? 39Ni lini tulikuona ukiwa mgonjwa au mfungwa nasi tukaja kukutazama?’
40 Mfalme atawajibu, ‘Kweli nawaambieni, kila kitu mlichomtendea mmojawapo wa hawa ndugu zangu wadogo, mlinitendea mimi.’
Sasa basi ni nini cha kufanya:
1. Tufanye matendo mema;
2. Tuache matendo mabaya;
3. Kama tumesahau kabisa, tusitende dhambi
Matendo mema ni yapi:
Mathayo 5
Hotuba mlimani
1. Yesu alipoyaona makundi ya watu, alipanda mlimani, akaketi. Wanafunzi wake wakamwendea,2. naye akaanza kuwafundisha:
Furaha ya kweli
3. “Heri walio maskini rohoni,maana ufalme wa mbinguni ni wao.4. Heri walio na huzuni,maana watafarijiwa.
5. Heri walio wapole,maana watairithi nchi.
6. Heri wenye njaa na kiu ya kufanya atakavyo Mungu,maana watashibishwa.
7. Heri walio na huruma,maana watahurumiwa.
8. Heri wenye moyo safi,maana watamwona Mungu.
9. Heri wenye kuleta amani,maana wataitwa watoto wa Mungu.
10. Heri wanaoteswa kwa sababu ya kufanya atakavyo Mungu,maana ufalme wa mbinguni ni wao.
11. “Heri yenu nyinyi watu wakiwatukana, wakiwadhulumu na kuwasingizia kila aina ya uovu kwa ajili yangu.
12. Furahini na kushangilia maana tuzo lenu ni kubwa mbinguni. Hivyo ndivyo walivyowadhulumu manabii waliokuwako kabla yenu.
Chumvi na Mwanga
13. “Nyinyi ni chumvi ya dunia. Lakini chumvi ikipoteza ladha yake itakolezwa na nini? Haifai kitu tena, ila hutupwa nje na kukanyagwa na watu.14. “Nyinyi ni mwanga wa ulimwengu! Mji uliojengwa juu ya mlima hauwezi kufichika.
15. Wala watu hawawashi taa na kuifunika kwa debe, ila huiweka juu ya kinara ili iwaangazie wote waliomo nyumbani.
16. Vivyo hivyo, ni lazima mwanga wenu uangaze mbele ya watu, ili wayaone matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.
Kuhusu sheria
17. “Msidhani kuwa nimekuja kutangua sheria na mafundisho ya manabii. Sikuja kutangua bali kukamilisha.18. Kweli nawaambieni, mpaka hapo mbingu na dunia zitakapopita, hakuna hata nukta moja au sehemu ndogo kabisa ya sheria itakayoondolewa, mpaka yote yametimia.
19. Basi, yeyote atakayevunja hata amri moja ndogo kuliko zote, na kuwafundisha wengine wafanye hivyo, huyo atakuwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni. Lakini yule atakayezishika na kuwafundisha wengine, huyo atakuwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni.
20. Ndio maana nawaambieni, wema wenu usipozidi ule wa waalimu wa sheria na wa Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.
Matayo 22:34-40
Amri Kuu Kuliko Zote
34 Mafarisayo waliposikia kwamba Yesu alikuwa amewanyamazi sha Masadukayo, walikutana wakamjia pamoja. 35 Mmoja wao, mtaalamu wa sheria akajaribu kumtega kwa kumwuliza, 36 “Mwali mu, ni amri ipi iliyo kuu kuliko zote?”37 Yesu akamjibu, “Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote na kwa akili zako zote.’ 38 Hii ndio amri kuu, tena ni ya kwanza. 39 Na ya pili inafanana nayo, nayo ni hii: ‘Mpende jirani yako kama nafsi yako.’ 40 Amri hizi mbili ndio msingi wa sheria zote na Maandiko ya manabii.”