Naomba serikali ituruhusu tulime bangi Ila tuuze nje na kuwe na udhibiti

Naomba serikali ituruhusu tulime bangi Ila tuuze nje na kuwe na udhibiti

Superbug

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2018
Posts
13,864
Reaction score
35,079
Naiomba serikali ituruhusu tulime bangi Ila tuuze nje Mimi ni mkulima wa mahindi na mpunga Nina jumla ya hekta 290 Ila za mahindi ni 150.

Kilimo cha mahindi kimenitia hasara Sana na kwa mwaka huu mbolea imepanda mno mfuko wa kilo 50 unauzwa laki na ishirini nahisi naenda kufilisika.

Ila serikali ikiruhusu tulime bangi itapata Kodi kubwa na pia iweke udhibiti wake ili kuzuia cartels Kama za Mexico.
 
Bangi sio mbaya Ila utumiaji wake Kama sisi tunaiogopa Basi tu export nje naumia Sana nikiona jamaa zangu Zimbabwe wanatajirika halafu Mimi nakuwa maskini.
 
Kama Kuna wadau wako humu na wanaoweza kuisaidia serikali kukokotoa faida vs hasara zake plz watusaidie kuishawishi serikali.
 
Bangi ni utajiri tunaoukali Yani ng'ombe wa maskini hazai.
 
Mafuta ya bangi nimesikia yanasaidia sana kurekebisha mapafu yaliyo na hitilafu hata kifua cha mshipa.

Hii bangi ikiruhusiwa tutaiuza Kenya maana wao ndiyo waenya Kiingilishi cha kutafuta masoko Ulaya.
 
Mfano mzur chemikali aina ya CBD ni maarufu kwaajili ya kutengenezea dawa za maumivu kama sikosei na mafaida mengne kibao ambayo cyafaham.

So ni dhahiri kwamba bangi pesa iliyokaliwa na upumbavu wa watanzania.

Maendeleo ya Tanzania mpya ni BANGI.
 
Masoko yote maarufu ya mtandaoni (ebay,Amazon, Alibaba) kuna products zitokanazo na bangi na tunaagiza mpaka wabongo wenyewe bila shida na bidhaa zinapita hapo Airport tunaletewa hadi mikoani na Shirika la Posta.😁

Kama tumewaruhusu wachina wachinje punda na ku-pack kwa soko la nje hata bangi inawezekana.

Bangi sio mbaya Ila utumiaji wake Kama sisi tunaiogopa Basi tu export nje naumia Sana nikiona jamaa zangu Zimbabwe wanatajirika halafu Mimi nakuwa maskini.

Weka picha ya mjani ili ulitendee haki jukwaa letu la picha...
 
Kuna Mbunge Mwaka juzi alishawahi kupendekeza hili Bungeni, kwa jina nafikiri Mbunge huyo anaitwa Jumanne
 
Ukiruhusu bangi ilimwe kwa export trade pia utatakiwa kila mkoa ujenge hositali za "MIREMBE". kwani bangi nyingi itazagaa mitaani kama pipi, inatakiwa kupima pros and cons in national rather than individual level kabla hujaamua kitu kama hicho.
 
Kama sasa hivi inazuiwa na bado watu wanavuta bila serikali kupata chochote, bora utaratibu uwekwe wstakaotaka kuwekeza, wapige pesa na wale wanaotaka kuvunja sheria waendelee kuvuta kama wanavyovuta sasa hivi.
 
Mkuu, utakaporuhusu nchinni ulevi wenye madhara permanent kichwani basi ni sawa na kuua taifa, naam kwa kuwekeza katika hiyyo biashara wapo watakao faidika na serikali itapata kodi, kodi ambayo mwisho wa siku itatumika kwa ajili kutibu vichaa waliotokana uvutaji bangi, kumbuka pia ukihalalisha hiyo biashara watu wengi wataanza kuhamasika kuvuta na hapo utajenga taifa la WAVUTA BANGI, Angalia Philadelphia Kensington street huko Marekani jinsi watu wake walivyoathirika na madawa ya kulevya kiasi kwamba Street hiyo inaitwa ZOMBIE LAND.
 
Back
Top Bottom