So far, comments and reactions for this thread seems to be based, mostly on fear of what might happen if that comes true or to learn new things that comes our way or even new ideas that are quite different to what we used to or taught in our schools, its very sad, if you, being the Citizen of the Information Age, with each and every thing at your disposal to confirm any information you receive can have such kind of fear, its very sad, remember, Fear is the biggest enemy to success, we need to overcome, it if we really mean it, wanasema Uoga wako ndio umasikini wako!
Watanzania hatuna budi kuchukua hatua za makusudi kama kweli tuna uchungu na maisha yetu na uchu mi wetu binafsi pia, kulalamika hakutatusaidia hata kidogo, tuamke, hatuwezi fika mbali kama tutakalia porojo tu, kinachoonekana hapa ni kilio cha kuhofia shilingi isishuke kufikia hapo, lakini jiulize wewe binafsi wafanya nini katika hili?
Tubadilike, tujitume, tukamate na kujaribu kila fursa zilizopo mbele yetu kwa maendeleo yetu sote, kukaa na kulaumu serikali hakutatusaidia hata kidodo, tuache majungu, hayajengi, hatuwezi kuendelea kuwa nchi ya "Pool, Simu na Pombe" (msemo wa mwana JF mmoja) naongezea na UDAKU (kwa hili la udaku huitaji kufanya utafiti mkubwa, nenda meza za magazeti angalia yanayonunuliwa sana kisha njoo hapa JF angalia sred zinazochangamkiwa utapata jibu) alafu tukatarajia muujiza wa Shilingi yetu kupanda, haiwezekani, ni kujidanganya, hatuwezi kubadirika bila kubadili fikra na mitazamo yetu kuhusu fursa mbali mbali zitujiavyo, ni ndoto.
Hatuwezi kufanya shilingi yetu ipande kwa kuendekeza viti virefu, pool, simu na kushabikia UDAKU, haiwezekani, tutairaumu serikali bure tu, tutaria kilio cha samaki, machozi yataenda na maji, Zama za kutarajia serikali, shirika, mwajiri au kampuni ikufanyie kila kitu maisani mwako imepita, haiko tena, ya sasa ni juu yako binafsi kujitengenezea uchumi na taratibu zako binafsi, ndio maana wengi wamelalama kusikia dada yule akiomba vile, sio kosa lake, kuna kitu ameaona, wewe na usomi wako hutaki kukiona, atakusaidiaje? Amka, chukua hatua kabla jua halijakuchwa.