Naomba tafsiri ya neno 'entertainment'.

Naomba tafsiri ya neno 'entertainment'.

mpendwa789

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2013
Posts
226
Reaction score
110
Naomba tafsiri ya sentensi hii:

Some churches are no longer places of worship, instead they have become places of entertainment (in order to attract people).

Hasa napenda kujua tafsiri ya neno ‘entertainment'

Nilijaribu kutafsiri kama ifuatavyo:

Makanisa mengine yaliacha kuwa mahali pa ibada, badala yake yamekuwa mahali pa ……………………………. (ili yaweze kuwavuta watu tu.)

Nimeshindwa kutafsiri vizuri neno ‘entertainment'! Kamusi inatoa maneno mengi lakini sijui lipi linahusu sentensi hiyo! Namaanisha ya kwamba makanisa kadhaa yanatumia muziki na vyombo vya kisasa (vya kelele sana) pamoja na waimbaji wanaoimba kana kwamba wapo runinga (televisheni).

Pia kwa context hii ningependa kujua vipi kutafsiri verb ‘to entertain' kwa sentensi hii:

‘Some churches just want to entertain people.'

Asanteni!
 
Nitajaribu. Kwa swali lako inaelekea maneno ya karibu sana ni:
Entertain = Kirimu, burudisha, furahisha. Angalia kwenye swali lako nimekujibu. Nategemea hii itasaidia.


Naomba tafsiri ya sentensi hii:

Some churches are no longer places of worship, instead they have become places of entertainment (in order to attract people).

Hasa napenda kujua tafsiri ya neno ‘entertainment’ = Burudani

Nilijaribu kutafsiri kama ifuatavyo:

Makanisa mengine yaliacha kuwa mahali pa ibada, badala yake yamekuwa mahali pa ... burudani.... (ili yaweze kuwavuta watu tu.)

Nimeshindwa kutafsiri vizuri neno ‘entertainment’! Kamusi inatoa maneno mengi lakini sijui lipi linahusu sentensi hiyo! Namaanisha ya kwamba makanisa kadhaa yanatumia muziki na vyombo vya kisasa (vya kelele sana) pamoja na waimbaji wanaoimba kana kwamba wapo runinga (televisheni).

Pia kwa context hii ningependa kujua vipi kutafsiri verb ‘to entertain’ kwa sentensi hii:

‘Some churches just want to entertain people.’ Baadhi ya makanisa yana malengo ya kuwaburudisha (au kutoa burudani) kwa watu tu.

Asanteni!
 
Kamusi ya kiingereza kwenda kiswahili itakupa maana kamili
 
Kamusi ya kiingereza kwenda kiswahili itakupa maana kamili

Kamusi ya kiingereza kwenda kiswahili inanipa maana yafuatayo kwa ‘entertainment':

machangamko
vichekesho
mandari
michezo
raha
tafrija
tamasha
uhondo
vitumbuizo
burudani
posho za tafrija
takrima
rasma

pamoja na maneno haya kwa ‘to entertain'

kuburudika
kufurahisha
kukirimu
kustarehesha
kutumbuiza

Kwa hiyo nilichanganyika nitumie neno lipi kwa context hii! Najua lugha ya Kiingereza lakini ninajifunza lugha ya Kiswahili! Kwa hiyo niliuliza.

Kwa kweli inaonekana ‘burudani' ni bora kwa context hii!

Asanteni!
 
Nitajaribu. Kwa swali lako inaelekea maneno ya karibu sana ni:
Entertain = Kirimu, burudisha, furahisha. Angalia kwenye swali lako nimekujibu. Nategemea hii itasaidia.

Asante sana! Nakushukuru!
 
Back
Top Bottom