Naomba TANROADS na mamlaka nyingine husika kuiwekea matuta Akachube Road, ajali zimezidi

Naomba TANROADS na mamlaka nyingine husika kuiwekea matuta Akachube Road, ajali zimezidi

N'yadikwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2014
Posts
7,427
Reaction score
10,905
Tunaomba tafadhali muweke matuta. Watoto wanagongwa na watu wazima wanajeruhiwa. Barabara ni nzuri sana na nyoofu ila madereva wanalala mbele sana kwenye barabara hii na ukizingatia iko mtaani 'uswazi' watoto wafyekwa kwelikweli hapa. Hivi juzi akina mama waliweka mawe hapo barabarani.

Nami naomba muweke matuta kuwadhibiti madereva hawa.
 
Issue siyo matuta kwani yanasababisha uharibifu wa magari na kuharibu mwonekano mzuri wa barabara, cha msingi waweke alama nzuri za tahadhali, mfano "alama za kudhibiti mwendo" mara tu uingiapo katika barabara hiyo, End!
 
Hakuna haja ya matuta
Mkimkamata mtu aliyegonga mtu
Mshikishen adabu mtundikeni juu
Iwe fundisho kwa wengine
Mambo ya kutoboa lami na kuweka matuta ni uaribifu tu wa barabara

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii tabia ya kutaka kila barabara kuwekwa matuta eti kisa kuna mtu aligongwa pale tuache mara moja. Mkitaka kujua namna matuta yanavyoharibu uzuri wa barabara na kuharibu magari ya watu piteni barabara ya Tunduma - Sumbawanga. Watembea kwa miguu na madereva tukiheshimu alama za barabarani hakutakua na ajali za kizembezembe kama ilivyo kwa sasa. Wazazi wanawaachi watoto wacheze watakavyo ilihali wanajua kua hawana elimu ya kutosha ya matumizi ya barabara.
Nilishangaa pale buguruni sheli, kumejengwa daraja la juu kwa ajili ya watembea kwa miguu kuvuka barabara lakini watu hawataki kulitumia na matokeo yake pale junction chini taa zinaruhusu au trafiki anaruhusu magari yanakuja kwa kasi mara unaona kundi la watu ghafla linakuja vuu wameingia barabarani eti wanavuka alafu wanataka usimame na ikitokea umemgonga mtu pale unapigiwa kelele kibao na ukinusurika kipigo cha raia unashukuru Mungu. Kwa sasa huwezi kuleta gari fupi sana maana hutopata sehemu ya kuiensha. Mbona kwa wenzetu chi zilizo nyingi hakuna hayo matuta ya hovyo na watu hawagongwi na magari hovyo hovyo. Tuache mambo ya kizamani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom