Pole sana ndugu yangu.
Kwanza nikutie moyo kwamba tatizo lako linaweza kupona kirahisi kabisa ondoa hofu. Kwa faida yako na wengine wenye interest na jambo hili,napenda kuzungumzia mambo kadhaa kabla sijakuambia ukamwone daktari.
Kwanza ondoa wazo la kwamba fungus imo kwenye damu. Uwezekano wa fangus kuishi kwenye damu(systemic) kipindi chote hicho ni mdogo sana;na hata hivyo dalili zake zisingekuwa kujikuna sehemu moja(local) tu. Ni wazi tatizo litakuwa hapo hapo unapojikuna.
Kuna mambo kama matatu hivi yanayopelekea mgonjwa kuchelewa kupona au kutopona kabisa.Kwanza,ikiwa mgonjwa anatumia dawa ambayo haihusiani na tatizo lake,mfano,mtu ana muwasho unaosababishwa na uchafu au sababu nyingine,halafu anapewa dawa ya fungus;kwa kweli hata akihamishia nyumbani pharmacy nzima ya dawa za fungus,itakuwa ni ndoto kupona.
Pili,ikiwa mtu anatumia dawa sahihi lakini kwa dose ambayo sio sahihi,pia hawezi kupona.Kwa mfano,dawa inatakiwa itumike mara tatu kwa siku(24hrs),yeye anatumia mara mbili tu,au dawa inatakiwa itumike kwa wiki 4,yeye anatumia dawa kwa siku 5 au 7 tu,hapo napo itakuwa ngumu kupona.
Lakini pia inaweza ikawa dawa ni sahihi kwa ugonjwa ule,na dose pia ni sahihi,lakini akashindwa kufuata masharti ya kutumia dawa ile.Ktk hili inawezekana mgonjwa ameshindwa mwenyewe kwa makusudi,au daktari hakumwambia kama kuna masharti ambayo anatakiwa kufuata. Kwa mfano,masharti ya kutibu fungus kwenye sehemu za siri,ni lazima kubadilisha/kusafisha underwear kila unapokuwa umepaka dawa;ili usijiambukize tena kupitia hiyo/hizo nguo.Kama utashindwa kusimamia hayo masharti,lazima kupona kwako kutazorota.
Nimetoa maelezo haya kwa nini? Mara nyingi wagonjwa na pengine hata baadhi ya madaktari wamekuwa wakitumbukia ktk mtego huo. Sasa ni vema basi ukajua kwamba si dawa tu,bali kuna mambo mengi ya kuzingatia wakati wa matibabu. Kitaalamu,mara nyingi matibabu ya fungus,yanatakiwa kwenda hadi mwezi mzima,lakini uzoefu unaonesha kwamba watu wengi hawafikii huko. Na hii ni kwa sababu dawa nyingi/cheap za fungus ktk mazingira yetu ni za tube,kwa hiyo mtu akinunua tube moja anatarajia kwamba akiimaliza ndio anakuwa amepona. Na ndio maana asipopona ataenda atanunua tena dawa(tube) nyingine tofauti ambayo nayo atatumia hadi itakapoisha. Kwa hiyo kanakuwa kamchezo fulani ka kubadilisha tubes kila mara. Mwisho wa siku mtu anaanza kupanic kwamba hili ni gonjwa gani lisilopona,kama ambavyo mwenzetu leo umeamua kuvunja ukimya!
Tatizo lingine ni kwamba watu wengi wanapenda sana kutibiwa kwenye maduka ya dawa badala ya kwenda hospitali angalau kufanyiwa uchunguzi.Sisemi watu wasipate huduma ktk maduka ya dawa,hapana. Ila kusema kweli hata mimi ninamiliki maduka kadhaa ya dawa,lakini kiukweli ninajua uwezo/utaalamu wa wahudumu wa haya maduka yetu!Ni bahati mbaya kwamba hayafanyi kazi kulingana na makusudio yake.Anyway,sitaki kwenda mbali zaidi ktk hili,maana linahitaji muda wa kutosha kulijadili.
Kwa leo itoshe tu kusema,ndugu yangu wewe nenda ktk hospitali iliyo karibu na wewe,utakutana na daktari atakufanyia uchunguzi kisha utapewa dawa na masharti(kama yapo),ukijisimamia vizuri,tatizo lako litakwisha kabisa.
Asanteni sana wakuu.