Naomba tofauti ya Lengo na Dhumuni

Naomba tofauti ya Lengo na Dhumuni

Yacn006

New Member
Joined
Sep 27, 2018
Posts
3
Reaction score
4
Naomba nipate msaada juu ya hili kuna tofauti yoyote juu ya maneno haya LENGO na DHUMUNI
 
Lengo ni yale mambo ambayo umejipangia ili uje uyatimize,mfano "nalima shamba kwa lengo la kuja kupanda mahindi"
"Naweka fedha kwa lengo la kuja kununua gari" "Lengo langu ikifika mwaka fulani nitajenga nyumba"

Dhumumi ni kusudio au sababu ya unalolifanya kwa wakati huo,mfano "Dhumuni langu la kuja hapa ni kuwajulia hali" so, lengo ni ile plani ya muda mrefu na dhumuni ni lengo la muda mfupi,

Nimejaribu,wataalamu watakuja kuongezea.
 
Sijaelewa kwann umetumia tena neno LENGO wakati unazungumzia DHUMUNI

uliposema dhumuni ni LENGO la muda mfupi
 
Wakati ulipokuwa Shule inaonekana mwalimu wako alikuwa anapata shida sana..
 
1).lengo;Ni nia/kusudi kuhusu Jambo fulani.
✓kwa mfano,lengo langu Ni kufahuru mtihani wa kidato ch sita.
Lakini;
2).Dhumuni;Ni matarajio/sababu kuhusu kitu fulani.
✓kwa mfano, Dhumuni la kuandika barua hii nikutaka kukujulia hali.
 
Back
Top Bottom