Naomba tujadili utawala wa Magufuli tukiweka kando itikadi zetu za kisiasa

anataka kuigeuza tz kuwa kama malaysia kwa kujenga taa za barabarani chato
 
Umasikini wa afrika imesababishwa kimakusudi na watawala lengo kuu ni kuwafanya watawaliwe coz hawana confidence ya kuongoza wasomi na matajiri thus ujiona wapo salama zaidi kutawala masikini Future less people.
Mkoloni alikuja kumkomboa mwafrika wapigania Uhuru wakamrudisha mwafrika utumwani. Maisha ya waafrika yamekuwa ya hovyo Sana baada ya Uhuru kuuliwa, kubambikwa, magonjwa, Vita, ukosefu wa ajira. Huku kundi la watu wachache ndilo likifaidi matunda ya Uhuru.
Tupo radhi kununua v8 moja ni sawa na trekta 6 tena brand new hp 75 ambazo trekta 6 zingeleta ajira za kutosha shambani.
 
Mimi sio mwanachama wa chama chochote ila naipenda CHADEMA. Uchaguzi uliopita niliimpigia kura Tundu Lissu na uchaguzi wa 2015 nilimpigia kura Lowassa.

Binafsi naamini kwenye utendaji na uchapa kazi Magufuli anawazidi wakina Lowassa na Lissu. Anayoyafanya Magufuli nina uhakika Lowassa na Lissu hawawezi kuyafanya.

Kwa huu uchapakazi wa Magufuli (na kama factors zingine ambazo nitaziongelea hivi punde angejiepusha nazo) haki ya Mungu Tanzania ingekuwa kama Malasyia au South Korea au kama nchi zingine zilizoendelea kwa kasi ya ajabu.

Watu mnaweza kujiuliza "kwa nini nimekuwa nikichagua upinzani kwenye kila uchaguzi?" Jibu langu ni fupi tu. Siipendi ccm toka moyoni. Umaskini wote tulionao watanzania umesababishwa na CCM.

Mimi nimezaliwa kijijini na miaka yangu ya utotoni nimeishi kijijini kabla sijapata ufahamu nakuamua kukimbilia mjini hatimae kufanikiwa kuondoka Tanzania.

Vijijini kuna ufukara wa kutisha. Kuna familia ni kama zimetengwa na jamii kwa sababu ya ufukara. Kuna jamii za Kitanzania, amini usiamini bado zinaishi kama wanyama.

Hazina ustaarabu na uelewa kuwa binadamu wote ni sawa. Kila binadamu ana mwili wa nyama hivyo maumivu ya kumtendea mwenzako uovu ni sawa na yale wewe ungeumia kama ungetendewa.

Nimeshuhudia mara nyingi sungusungu wakiua mtu kwa fimbo kisa kaiba ngo'mbe. Huu ni mfano mmoja wapo kuwa kuna jamii bado hazijastaarabika na zinaishi kama wanyama.

Mfano mwingine kuna familia vijijini ni fukara kabisa, sijui nielezaje ili nieleweke. Kuna familia fukara ambazo watoto ni kama vile watoto wamejizaa. Utotoni mwangu nimechunga ng'ombe.

Huko machungani kuna familia unaweza ukamkuta mtoto wa kike mwenye miaka 7 anakaa na bibi yake asiyejiweza, wanakaa kwenye nyumba ya nyasi iliyoraruka isiyo na matumaini yoyote ya uhai wa mtu.

Familia inashindia mlenda na ugali wa mtama. Haina chochote hata kuku. Haya matatizo yote nikiyafikiria naona yamesababishwa na CCM.

Wakuu wa wilaya walikuwa wanakuja vijijini wakiwa na matumbo makubwa na vipara wakiendeshwa kwenye magari ya kifahali wakati jamii inaishi kwenye ufukara uliotopea. Hii ndio sababu kwa nini siipendi CCM.

Turudi kwa Magufuli. Magufuli ni mchapa kazi, tena sana. Kama ni Rais huyu ndio rais watanzania tulikuwa tunamhitaji. Kwa huu utendaji wake, angejiepusha na kasoro ya kukandamiza demokrasia angeifikisha nchi mbali sana.

Kinachomharibia Rais wetu ni chuki dhidi ya wapinzani. Laiti angefanya huu uchapakazi bila kukandamiza wapinzani, na kutoa uhuru kwa vyombo vya habari na taasisi zisizo za kiserikali, haki ya Mungu Tanzania ingekuwa level nyingine.

Magufuli kwa huu utendaji wake hakuna mpinzani angemshinda kwenye sanduku la kura kama asingekandamiza demokrasia. Binafsi hata mimi japo mara zote nimekuwa nikiwapigia kura wapinzani lakini nilikuwa natamani ashinde. Simpigii kura lakini natamani ashinde. CCM ndio siipendi ila Magufuli nampenda.

Naomba nihitimishe kwa kusema kwamba Magufuli laiti angeachana na mambo ya kukimbizana na wapinzani, akaweka mahusiano mazuri na jumuia za kimataifa hakika Tanzania ingekuwa level nyingine.

Demokrasia ingemsaidia sana kwenye uchapakazi wake. Jumuiya za kimataifa zingemuunga mkono hivyo jitihada zake zingekuwa na back up kutoka sehemu nyingi tofauti na sasa anapambana peke yake.

Naomba kuwasilisha.
Shida ya upinzani wa kiafrica sio upinzani wa kweli wanatumika na mabeberu kupinga maendeleo ya nchi na kupotosha watu wachache kama wewe ili muwafate. Ndomana Magu hata acha kuwandama ili wawe na akili timamu ya kujenge nchi na si kupinga pinga bila akili.
 
Ulivyotaka tu kuifananisha Tanzania na South Korea hapo hapo ndio nimekuupuza na sijaendelea zaidi kusoma huu ugoro wako.

Hao Nigeria tu hawasubutu kutaka kujifananisha na South Korea.

Yani watu watengeze Samsung na bado wawe na watu maboya kama wagogo?

Labda kuifanya Chato ifanane na Dar inawezekana.
 
Mimi sio mwanachama wa chama chochote ila naipenda CHADEMA. Uchaguzi uliopita niliimpigia kura Tundu Lissu na uchaguzi wa 2015 nilimpigia kura Lowassa.

Binafsi naamini kwenye utendaji na uchapa kazi Magufuli anawazidi wakina Lowassa na Lissu. Anayoyafanya Magufuli nina uhakika Lowassa na Lissu hawawezi kuyafanya.

Kwa huu uchapakazi wa Magufuli (na kama factors zingine ambazo nitaziongelea hivi punde angejiepusha nazo) haki ya Mungu Tanzania ingekuwa kama Malasyia au South Korea au kama nchi zingine zilizoendelea kwa kasi ya ajabu.

Watu mnaweza kujiuliza "kwa nini nimekuwa nikichagua upinzani kwenye kila uchaguzi?" Jibu langu ni fupi tu. Siipendi ccm toka moyoni. Umaskini wote tulionao watanzania umesababishwa na CCM.

Mimi nimezaliwa kijijini na miaka yangu ya utotoni nimeishi kijijini kabla sijapata ufahamu nakuamua kukimbilia mjini hatimae kufanikiwa kuondoka Tanzania.

Vijijini kuna ufukara wa kutisha. Kuna familia ni kama zimetengwa na jamii kwa sababu ya ufukara. Kuna jamii za Kitanzania, amini usiamini bado zinaishi kama wanyama.

Hazina ustaarabu na uelewa kuwa binadamu wote ni sawa. Kila binadamu ana mwili wa nyama hivyo maumivu ya kumtendea mwenzako uovu ni sawa na yale wewe ungeumia kama ungetendewa.

Nimeshuhudia mara nyingi sungusungu wakiua mtu kwa fimbo kisa kaiba ngo'mbe. Huu ni mfano mmoja wapo kuwa kuna jamii bado hazijastaarabika na zinaishi kama wanyama.

Mfano mwingine kuna familia vijijini ni fukara kabisa, sijui nielezaje ili nieleweke. Kuna familia fukara ambazo watoto ni kama vile watoto wamejizaa. Utotoni mwangu nimechunga ng'ombe.

Huko machungani kuna familia unaweza ukamkuta mtoto wa kike mwenye miaka 7 anakaa na bibi yake asiyejiweza, wanakaa kwenye nyumba ya nyasi iliyoraruka isiyo na matumaini yoyote ya uhai wa mtu.

Familia inashindia mlenda na ugali wa mtama. Haina chochote hata kuku. Haya matatizo yote nikiyafikiria naona yamesababishwa na CCM.

Wakuu wa wilaya walikuwa wanakuja vijijini wakiwa na matumbo makubwa na vipara wakiendeshwa kwenye magari ya kifahali wakati jamii inaishi kwenye ufukara uliotopea. Hii ndio sababu kwa nini siipendi CCM.

Turudi kwa Magufuli. Magufuli ni mchapa kazi, tena sana. Kama ni Rais huyu ndio rais watanzania tulikuwa tunamhitaji. Kwa huu utendaji wake, angejiepusha na kasoro ya kukandamiza demokrasia angeifikisha nchi mbali sana.

Kinachomharibia Rais wetu ni chuki dhidi ya wapinzani. Laiti angefanya huu uchapakazi bila kukandamiza wapinzani, na kutoa uhuru kwa vyombo vya habari na taasisi zisizo za kiserikali, haki ya Mungu Tanzania ingekuwa level nyingine.

Magufuli kwa huu utendaji wake hakuna mpinzani angemshinda kwenye sanduku la kura kama asingekandamiza demokrasia. Binafsi hata mimi japo mara zote nimekuwa nikiwapigia kura wapinzani lakini nilikuwa natamani ashinde. Simpigii kura lakini natamani ashinde. CCM ndio siipendi ila Magufuli nampenda.

Naomba nihitimishe kwa kusema kwamba Magufuli laiti angeachana na mambo ya kukimbizana na wapinzani, akaweka mahusiano mazuri na jumuia za kimataifa hakika Tanzania ingekuwa level nyingine.

Demokrasia ingemsaidia sana kwenye uchapakazi wake. Jumuiya za kimataifa zingemuunga mkono hivyo jitihada zake zingekuwa na back up kutoka sehemu nyingi tofauti na sasa anapambana peke yake.

Naomba kuwasilisha.
Nakuelewa unachosema, naielewa pia dilemma yako.
1) Nianze na hiyo hali ya ufukara huko usukumani. Hivi nikuulize, ni ccm ambayo imewafanya wazee wa kisukuma, kwa miongo mingi tu, kutumia fedha nyingi walizopata baada ya kuuza pamba, kwa anasa, kuoa, ufahari wa kishamba, kumwambia mhindi nipe baiskeli ya sh. 200 (enzi hizo), na mhindi anaongeza saiti mira na mapambo mengine kwenye baiskeli?
Bila shaka sio ccm iliyowafanya wazee wa kichaga kutumia mapato yao toka mauzo ya kahawa, kusomesha watoto wao Makerere, Nairobi na Ulaya.
Hata Tabora kule Unyamwezini, kwa miongo mingi wametumia fedha nyingi kwa makahaba wa kidigo na kibondei huko Tanga, baada ya kuuza Tumbaku. Wanarudi msimu mpya wa kulima Tumbaku unapoanza. Familia zao zikiishi katika ufukara mkubwa

2) Najua madhambi ya ccm, wala mimi siwapigii kura ccm, lakini tuwe wakweli, na tujue tatizo liko wapi.

Magufuli huwezi kumtenganisha na udikteta, kuchukia kukosolewa, na kujiona kama ni mfalme. Anachofanya Magufuli ni hatari sana kwa mustakabali wa taifa letu. Anavunja instruments za demokrasia, kwa kutudanganyia peremende inaitwa "maendeleo". Hatuhitaji ushamba wakununua midege ile yote kwa sasa. Watanzania hawana maji, na wanahitaji kuwezeshwa ili wajiletee maendeleo.

Elimu imevurugwa, vyuo vikuu sasa vinatakiwa kutoa "gawio" kwa serikali ikajenge barabara, badala ya production of knowledge.

Hatuhitaji "maendeleo" ya maonesho, bali maendeleo ya watu, yanayoenzi utu wa mtu.
 
Kuna jiwe na kuna MAGUFULI, unataka tujadili kipi?

Hutu boy angeheshimika sana kama angejali utu wa watu, lakini hii ngwe Ni ngumu Sana kwa Hutu boy, na huenda akawa mbaya na katili zaidi kuliko amba historia imeshawahi kushuhudia.

Kuna jiwe na kuna MAGUFULI, unataka tujadili kipi?

Hutu boy angeheshimika sana kama angejali utu wa watu, lakini hii ngwe Ni ngumu Sana kwa Hutu boy, na huenda akawa mbaya na katili zaidi kuliko amba historia imeshawahi kushuhudia
Hutu boy, kazi moja tu, kuteka kutesa, kufunga na kuua, Watanganyika tunaompinga.
Mungu atuepushilie nae mbali.
 
Ni utawala bora unaolinda msalahi ya wanyonge na kukomesha mafisadi na wala rushwa. Katika utawala huu tumeona nidhamu ikirudi katika taasisi mbali mbali za umma !
 
Mkuu kwa kiwango flani uliyoyasema ni ya kweli lakini kuna mahala umejichanganya na hivyo kupoteza maana nzima ya unachokiamini na kile usichokiamini!
1.Umesema unamkubali JPM kwa uchapa kazi wake , lakini waichukia CCM, Je wajua JPM ndiye mkt na kiongozi mkuu wa hicho chama?
Unajua kuwa matendo ya chama chochote huwa ndio maagizo na matendo ya mkt wake? Kama waamini ufukara wetu mchawi wake ni CCM basi hapo mkt wake kwa miaka 5 anachomokaje???
2.Huwezi kumlinganisha Lowassa /Lissu na JPM na ukapata tofauti ya kweli sababu hao wote hawajapata kuwa marais wa Tanzania, Hivyo hapo hakuna scale yoyote inayofit kama kipimo. JPM mlinganishe na kina Kikwete, Mwinyi , Mkapa huko sawa lakini sio akina Lissu au Lowassa, hawa hawajawahi kukamata serikali kama maamiri jeshi wakuu wa taasis zote za serikali!
3.Umesema bila matendo yake dhidi ya wapinzani . Tanzania ingekuwa mbali kimaendeleo, Lakini hapohapo unasema wamkubali,
Unamkubali vipi mtu anayetusababishia kuwa nyuma kimaendeleo?? Uzalendo wako uko wapi?
Kimsingi watanzania tunachotaka ni maendeleo hivyo kiongozi wetu ni lazima awe chachu ya hayo maendeleo.
Mtu anaweza kuwa na sifa nyingi nzuri lakini sifa moja mbaya ikamfanya apoteze zile sifa nyingine zote!
 
Mkuu shukrani kwa uchambuzi murua. Ningependa nikujibu baadhi ya hoja zako. 1 inawezekanaje kumpenda Magufuli ilihali naichukia ccm? Binafsi naichukulia ccm kama taasis ambayo Magufuli ameikuta. Kwa maana nyingine ubaya wa ccm umekuwepo hata kabla ya Magufuli, hivyo hata kama Magufuli asingekuwa mwenyekiti bado ccm ingekuwa mbaya. 2. mtu msafi akijiunga ccm haimaanishi na yeye atakuwa mchafu, ndio maana ccm wengi pia wanasomeshwa namba na Magu, hii inaonyesha kwamba kumbe jamaa hawakubali hata wana ccm wenzake. Ccm imetawala karibia miaka 60 lakini bado kuna matatizo makubwa sana ambayo ilitakiwa kuyatatua miaka mingi nyuma. Swala la maji safi na salama kwa mfano halikutakiwa kuwa changamoto katika karne hii. Cha kushangaza a basic need like water eti ndio swaga ya kuombea kura. Unaweza kuona ni namna gani viongozi wa ccm wa enzi hizo walivyosababisha maisha ya ufukara wa watanzania kwa kushindwa kuwajibika. Ukija kwenye miundo mbinu, ni miaka ya kikwete at least mikoa michache iliweza kuunganishwa kwa lami. Enzi hizo kutoka Dar hadi Mwanza kulikuwa hakuna lami. Ilikuwa unasafiri kwa siku tatu kutoka Dar hadi Mwanza kwa njia ya train. Swali la kujiuliza, ccm ilikuwa inafanya nini? Ukija kwenye elimu, shule za sekondari zilikuwa chache. Darasa zima anaweza kufaulu mtu mmoja au hakuna kabisa kwenda secondari. Ndio maana wajinga kibao tumejazana kwa sababu kulikuwa na nafasi chache za kusoma. Hii ni mifano michache tu kwa nini siipendi ccm.
 
Kipindi cha kampeni za mwaka huu kimetufundisha mengi.
Naghani hata viongozi walioko madarakani akiwemo Mh. Rais sasa anajuwa nini hasa Watanzania wanataka na nini hawataki.
Ni kipindi cha kurekebisha makosa na kusonga mbele.
Naamini tutafanikiwa.
 
Mimi sio mwanachama wa chama chochote ila naipenda CHADEMA. Uchaguzi uliopita niliimpigia kura Tundu Lissu na uchaguzi wa 2015 nilimpigia kura Lowassa.

Binafsi naamini kwenye utendaji na uchapa kazi Magufuli anawazidi wakina Lowassa na Lissu. Anayoyafanya Magufuli nina uhakika Lowassa na Lissu hawawezi kuyafanya.

Kwa huu uchapakazi wa Magufuli (na kama factors zingine ambazo nitaziongelea hivi punde angejiepusha nazo) haki ya Mungu Tanzania ingekuwa kama Malasyia au South Korea au kama nchi zingine zilizoendelea kwa kasi ya ajabu.

Watu mnaweza kujiuliza "kwa nini nimekuwa nikichagua upinzani kwenye kila uchaguzi?" Jibu langu ni fupi tu. Siipendi ccm toka moyoni. Umaskini wote tulionao watanzania umesababishwa na CCM.

Mimi nimezaliwa kijijini na miaka yangu ya utotoni nimeishi kijijini kabla sijapata ufahamu nakuamua kukimbilia mjini hatimae kufanikiwa kuondoka Tanzania.

Vijijini kuna ufukara wa kutisha. Kuna familia ni kama zimetengwa na jamii kwa sababu ya ufukara. Kuna jamii za Kitanzania, amini usiamini bado zinaishi kama wanyama.

Hazina ustaarabu na uelewa kuwa binadamu wote ni sawa. Kila binadamu ana mwili wa nyama hivyo maumivu ya kumtendea mwenzako uovu ni sawa na yale wewe ungeumia kama ungetendewa.

Nimeshuhudia mara nyingi sungusungu wakiua mtu kwa fimbo kisa kaiba ngo'mbe. Huu ni mfano mmoja wapo kuwa kuna jamii bado hazijastaarabika na zinaishi kama wanyama.

Mfano mwingine kuna familia vijijini ni fukara kabisa, sijui nielezaje ili nieleweke. Kuna familia fukara ambazo watoto ni kama vile watoto wamejizaa. Utotoni mwangu nimechunga ng'ombe.

Huko machungani kuna familia unaweza ukamkuta mtoto wa kike mwenye miaka 7 anakaa na bibi yake asiyejiweza, wanakaa kwenye nyumba ya nyasi iliyoraruka isiyo na matumaini yoyote ya uhai wa mtu.

Familia inashindia mlenda na ugali wa mtama. Haina chochote hata kuku. Haya matatizo yote nikiyafikiria naona yamesababishwa na CCM.

Wakuu wa wilaya walikuwa wanakuja vijijini wakiwa na matumbo makubwa na vipara wakiendeshwa kwenye magari ya kifahali wakati jamii inaishi kwenye ufukara uliotopea. Hii ndio sababu kwa nini siipendi CCM.

Turudi kwa Magufuli. Magufuli ni mchapa kazi, tena sana. Kama ni Rais huyu ndio rais watanzania tulikuwa tunamhitaji. Kwa huu utendaji wake, angejiepusha na kasoro ya kukandamiza demokrasia angeifikisha nchi mbali sana.

Kinachomharibia Rais wetu ni chuki dhidi ya wapinzani. Laiti angefanya huu uchapakazi bila kukandamiza wapinzani, na kutoa uhuru kwa vyombo vya habari na taasisi zisizo za kiserikali, haki ya Mungu Tanzania ingekuwa level nyingine.

Magufuli kwa huu utendaji wake hakuna mpinzani angemshinda kwenye sanduku la kura kama asingekandamiza demokrasia. Binafsi hata mimi japo mara zote nimekuwa nikiwapigia kura wapinzani lakini nilikuwa natamani ashinde. Simpigii kura lakini natamani ashinde. CCM ndio siipendi ila Magufuli nampenda.

Naomba nihitimishe kwa kusema kwamba Magufuli laiti angeachana na mambo ya kukimbizana na wapinzani, akaweka mahusiano mazuri na jumuia za kimataifa hakika Tanzania ingekuwa level nyingine.

Demokrasia ingemsaidia sana kwenye uchapakazi wake. Jumuiya za kimataifa zingemuunga mkono hivyo jitihada zake zingekuwa na back up kutoka sehemu nyingi tofauti na sasa anapambana peke yake.

Naomba kuwasilisha.

Hatuna upinzani tanzania, upinzani siyo kutukana serikari, siyo kuhujumu nchi, siyo kuhamasisha vurugu.
Tanzania hatuna vyama vya upinzani , tuna chama kimoja na matawi yake, tuna chama kinachotumiwa na mabeberu kutaka yachote rasilimali zetu.

Natuna wanaharakati njaa.
Nawasilisha.
 
bila shaka wewe ni green guard..bisha? yaan kwa uandishi huu huchomoki hahahhahah nimekunasa
 
Sasa utamlinganisha Magufuri na watu ambao hawajawahi kushika Urais? Kama Lowassa na Lissu wangekuwa wameshawahi marais binafsi ningekuunga mkono au nimgekukalia!
 
Hatuna upinzani tanzania, upinzani siyo kutukana serikari, siyo kuhujumu nchi, siyo kuhamasisha vurugu.
Tanzania hatuna vyama vya upinzani , tuna chama kimoja na matawi yake, tuna chama kinachotumiwa na mabeberu kutaka yachote rasilimali zetu.

Natuna wanaharakati njaa.
Nawasilisha.
Mbona raslimali hizo tuliwakabidhi Mabeberu kwa kusaini mikataba feki iliyofanywa kwa baraka zote za Serikali ya Chama pendwa? Ni huyo huyo mnayesema anataka kutumiwa na mabeberu kwa miaka mingi amepigania raslimali zetu mpaka akaishia kupigwa risasi! Kama hakuna Upinzani Chama pendwa kisingetumia mabavu ya Dola na vyombo vyake kubaki madarakani!
 
Back
Top Bottom