Naomba tupeane uzoefu wa kuishi nyumba moja na mama mkwe baba mkwe mashemji

Naomba tupeane uzoefu wa kuishi nyumba moja na mama mkwe baba mkwe mashemji

habari zenu wadau mm na baba watoto tulikua tunaishi ktk nyumba ya kupanga kwa muda wa miaka minne sasa ila anataka tukaishi kwao kwa kua kidogo kodi imepanda ili tusave tuweze kuanza kujenga makazi yetu sasa jamani naomba mnipe uzoefu wa kukaa na mama mkwe baba mkwe mashemeji na mawifi ndani ya nyumba mm nikiwa nina watoto wawili wadogo 3 years na 1 year mm ni mfanyakazi naenda kazini asubuhi jumatatu hadi ijumamosi siku yangu ni moja tu jumapili kiukweli mm sipo comfortable kuenda kulundikana kwenye nyumba moja yaani nipo nafuraha nikiwa naishi kwangu. si kama siwapendi ndugu wa mume lakini sipo comfortable. hebu nipeni mawazo yenu juu ya hii ishu.

naomba mwenye lugha ya kejeli afunge mdomo wake
Isifanye hiyo kitu ndgu yang kama unampenda mkeo...kufany hivo jua unamrudisha mkeo kwao ila we utaondokaa tu hapo

Sent from my TECNO-L8 using JamiiForums mobile app
 
Ukweli mchungu, aadhani hili pia ni jibu maana huenda dada hakuwa anampa support mme wake. Kama wote mnafaanya kazi hamuwezi kushindwa kulipia hilo pango ila kwa vile dada hapo pengine anamwachia kaka issue nyingi. Kama wadau walivyosema, jaribuni kutafuta nyumba yenye kodi ya chini mhame hiyo ya sasa.
SAPOTI NATOA sana na hata hili lilipokuja mm nikasema nitalipa mm hiyo kodi
 
ish

u ni kuwa unapokua umeshazoea kuishi kwako unakua na life style yako sasa unapokwenda sasa ukweni unatakiwa uanze kujitune upya nikiwa kwangu ninamaamuzi kuwaleo ni week end sipiki nataka kulala tuu hadi saa tatu sasa upo na wakwe utakuta watu wanaangali saa na kujiuliza hee fulani hadi saa hizi kalala yaani wanaume mnaona ni ishu ndogo lakini kwa ss wanawake kukaliana pamoja ni changamoto
Hapo Kwenye Mstari Yaani Mumeo Unamuachaga Na Njaa Hupikagi Unataka Ule Chipsi Ngoja Uende Ukwenu Ukasonge Kilo 10 Ya Ugali Na Zamu Ya Kupika,usafi Nk
 
"Limit your freedom, jimilikishe kwao"

Badilisha mtazamo wako, elewa kuwa we ni sehemu ya familia ya mme wako!

LoRd JeSuS ChRiSt - The Creator Of All.
 
Mhuuuuuu,kuna changamoto sana,kwanza hautakuwa na uhuru kama ulikokuwa nao kwako,bora mpange chumba na sebule huku mkijenga nyumba yenu kuliko kwenda kukaa ukweni.
 
Mwambie mumeo aache kuogopa maisha kwani kuna nyumba zenye gharama nafuu mwaweza kwenda kukaa huko kuliko kwenda kuishi ukweni. Usithubutu kwenda kuishi ukweni kwa kigezo cha kutaka kujenga, mwambie mwenzio akubaliane na changamoto za maisha mwaweza kuwa juu ama kushuka chini ila kikubwa ni kupambana.
Swadakta dada hayo maneno yako ni maneno kuntu anatakiwa asiogope maisha hata chumba kimoja akodi ila kuishi kwa wakwe kama hana sababu sio vizuri ila awe na sababu ya msingi hiyo siyo sababu kabisaaaaa madhali mume ana kazi ya kufanya na nguvu anazo kwa mm sitoweza

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Sijawahi kufikiria kuishi na wakwe kabisa katika paa moja. mwenzi wa kwanza uishe wa pili 3,4,5 hadi mwaka hapana kabisa.......... Haiwezekani kabisa

Dada uzuri una kazi hakuna linaloshindikana tafuta nyumba ya bei rahisi zaidi ya hiyo jibane acha kwenda kwa wakwe kabisa hata kama nyumba mmemjengea ninyi. Fanya juu chini lakini sio kwenda kuishi kwa wakwe kabisa...

Na pia jamani hata kama uko kwenye ujenzi sio ujibane mpk tone la mwisho
 
Kwa kweeli ni ngumu, ila sababu ni kwa muda na maisha yenyewe ndo haya inabidi iwe hivyo tuu...

Ni Sawa na kuishi na wazazi wako na kaka ama dada zako... Maisha yana changamoto mamy... Pambana nazo, kuwa wewe na utaona kila kitu kinawezekana.
 
Kazi unayo, ila ndio hivyo mume wamtaka, wafuate wasemavyo maana mji wao huo sio wako...
 
Hapo Kwenye Mstari Yaani Mumeo Unamuachaga Na Njaa Hupikagi Unataka Ule Chipsi Ngoja Uende Ukwenu Ukasonge Kilo 10 Ya Ugali Na Zamu Ya Kupika,usafi Nk

huu ni utaratibu ambao tunajiwekea ktk family kuwa week end baada ya mihangaiko ya wiki nzima tunatumia muda mwingi kupumzika then tanaendelea na ratiba za kila siku na nimetolea tu mfano na hata ikiwa nitalala hadi saa zote ni kuwa tayari huyu mume wangu anaelewa mazingira halisi ya kazi wiki nzima ni kitu cha kawaida unaamka unawali unaweka chai then tunarudi tunachapa usingizi sasa ratiba kama hii kwa wanaokuzunguka waweza kuitwa mvivu lakini sio uvuvi ni utaratibu ambao mtakua mmekubaliana mume na mke
 
Usiende my dia..watakufanya punda wadobi! na ole wako ukatae, katafute nyumba ya bei rahisi mbona zimeshuka bei mno kipindi hichi.
 
Ni ngumu na unaweza kujikuta hiyo hela mnayosave kwenye kodi ukamtafuta aunt Sadaka kwa counselling.

Itabidi uondoke kwenye comfort zone yako na J2 siku yako ya mapumziko itakuwa siku yako ya kupika lunch baada ya hapo unawaambia unahitaji kupumzika.

Maisha na mawifi na mama mkwe ni mazuri sana pale unapojua limit ya mdomo wako, 'she said this' zikianza nyumbani utapaona pachungu.

Positive side child care bibi atawalea wajukuu hata kama kuna dada atamkbusha kuogesha watoto.
 
Kazi unayo, ila ndio hivyo mume wamtaka, wafuate wasemavyo maana mji wao huo sio wako...

asante sana mm binafsi nimejenga nyumba ina 3 bedrooms but haina umeme mm nipo tayari kwenda tukaishi kwenye hii nyumba yangu lakini mume wangu hataki kwa kua anadai ni mbali sana usafiri tunao ila hayupo tayari kuishi ktk nyumba niliyoijenga
anataka tukaishi kwao kwa kua hiyo nyumba ya kwao aliijenga yeye ila ndio familia yote ipo humo mm nitakua na room yangu tu
yaani nachokaje sijawahi kugombana na mkwe au wifi wala shemeji naishi nao vizuri na wananipenda ila kwa kua tupo mbalimbali na nijelewa na uwezo wa kuyapuuza maudhi madogo kwa kua tulikua tupo mbali mbali sasa ninawaendea chini ya miguu yao

uuuwwwwwwiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
huu ni utaratibu ambao tunajiwekea ktk family kuwa week end baada ya mihangaiko ya wiki nzima tunatumia muda mwingi kupumzika then tanaendelea na ratiba za kila siku na nimetolea tu mfano na hata ikiwa nitalala hadi saa zote ni kuwa tayari huyu mume wangu anaelewa mazingira halisi ya kazi wiki nzima ni kitu cha kawaida unaamka unawali unaweka chai then tunarudi tunachapa usingizi sasa ratiba kama hii kwa wanaokuzunguka waweza kuitwa mvivu lakini sio uvuvi ni utaratibu ambao mtakua mmekubaliana mume na mke
Sasa Unachoogopa Nn Ukweni Ni Kama Nyumbani,kumbuka Umemfuata Mumeo Siyo Mama Yake Wala Dada Zake Kumbuka Siye Wanaume Hua Tunajua Mengi Hata Kama Ikitokea Sintofahamu Tunajua Jinsi Yakusawazisha Mambo Kama Hayo
 
Back
Top Bottom