Naomba uahauri na uzoefu; Nataka kuwa dalali

leonardbuba

Member
Joined
Nov 30, 2017
Posts
47
Reaction score
26
Nahitaji kujiajiri niwe dalali wa nyumba,mashamba viwanja,magari n.k
Sasa nilikuwa nahitaji ushauri na uzoefu ambao mnafahamu changamoto na jinsi ya kufanikisha ila nataka kufanya mkoani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Oooh so inabidi iwe kama kazi ya ziada

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndiyoo mkuu au uangalie hapo kwenye udalali iko fursa gani, maana udalali nao ni mgumu kama hujui jinsi ya kupata connection na watu, mfano wewe unaweza kujifunza jinsi ya kumake furniture, ufundi wa rangi au unaweza omba kazi afu unaita fundi, kwa hiyo unajitangaza kiivyo, maana kwenye nyumba utakutana na hizo deal, afu ebu komaa uwe na Usafiri hata pikipiki wa kumove sites.
 
Sawa ndgu Ahsante kwa ushauri mzuri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwisho kabisa ukiona mtu kafanikiwa kupitia biashara za udalali Kama haikuwa zali, Mara nyingi huwa ni dalali ambaye ameshibana na mmiliki wa Mali yaani unakuta wewe unarafiki tajiri sasa unamsaidia kuuza Mali zake au Mali yake kwa hiyo hapa dalali unaye muona saa ingine naye katoboa na hana Mali unakuta ni yule mwenye ukaribu kabisa na mmiliki either ndugu, rafiki au hata wadamu moja, chunguza hii utajua kwa mjini madalali wanao win wanakuwaga wa aina hii.

pia na dalali akiuza Mali Mara moja anainuka anakuwa Kama boss let say plot au nyumba, so connection ya mmiliki ni nguzo pia, maana mmiliki ndiyo mwenye mamlaka, owner of the assets... Mnaweza mkawa madalali wengi mkitafuta mteja sokoni afu mmliki unakuta anamfahamu rafiki yake dalali ukipeleka mteja unachinjiwa mbali...

Ndugu yangu udalali pia ni kufanya kazi kwa kujuana. Sasa ukiwa dalali wakati wako wote usitangaze Mali au kutafuta mteja ikiwa huna mahusiano au makubaliano mazuri na mmliki maana inaweza ikawa kazi bure kabisa.
Nikutakie hustle njema, maisha ni mapambano na juhudi shina la mafanikio....
 
aiseh
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…