Mwisho kabisa ukiona mtu kafanikiwa kupitia biashara za udalali Kama haikuwa zali, Mara nyingi huwa ni dalali ambaye ameshibana na mmiliki wa Mali yaani unakuta wewe unarafiki tajiri sasa unamsaidia kuuza Mali zake au Mali yake kwa hiyo hapa dalali unaye muona saa ingine naye katoboa na hana Mali unakuta ni yule mwenye ukaribu kabisa na mmiliki either ndugu, rafiki au hata wadamu moja, chunguza hii utajua kwa mjini madalali wanao win wanakuwaga wa aina hii.
pia na dalali akiuza Mali Mara moja anainuka anakuwa Kama boss let say plot au nyumba, so connection ya mmiliki ni nguzo pia, maana mmiliki ndiyo mwenye mamlaka, owner of the assets... Mnaweza mkawa madalali wengi mkitafuta mteja sokoni afu mmliki unakuta anamfahamu rafiki yake dalali ukipeleka mteja unachinjiwa mbali...
Ndugu yangu udalali pia ni kufanya kazi kwa kujuana. Sasa ukiwa dalali wakati wako wote usitangaze Mali au kutafuta mteja ikiwa huna mahusiano au makubaliano mazuri na mmliki maana inaweza ikawa kazi bure kabisa.
Nikutakie hustle njema, maisha ni mapambano na juhudi shina la mafanikio....