Naomba ufafanuzi juu ya kifaa cha microchip

Naomba ufafanuzi juu ya kifaa cha microchip

k

wani wewe ulivyosema mnyama hawezi kutanguliwa na chip kwenye comment yako ulikuwa unmaanisha mnyama yupi?
Hivi microchip haiwezi tangulia na kuandaa mazingira ya huo ufalme/mnyama?

Mbona nimeeleza kwenye maandiko yangu kuwa ni mnyama gani?

Kwenye Ufunuo 13 kuna wanyama wawili wamesemwa mule na mimi nazungumzia mnyama wa kwanza kwenye Ufunuo 13:1

Kuhusu microchip na kipi kitatangulia,
Kwanza unatakiwa ujue kwamba hakuna uthibitisho kuwa microchip ndiyo ile alama ya mnyama inayosemwa kwenye Ufunuo 13....

Nilichokifanya hapa nime assume kuwa hiyo microchip ndiyo hiyo alama ya mnyama.Kama ni hivyo haiwezi na haiwezekani uletewe alama ya kisichokuwepo au kuwahi kuwepo,kwanza kinaanza kile ambacho alama itakihusu ili wewe ujue hiyo ni alama ya nani au nini....

Isingeweza kuitwa alama au hesabu ya jina la mnyama kama mnyama huyo asingekuwa ameshajulikana maana maandiko yasingeweza kueleweka. Ni sawa na leo uletewe jina la kitu ambacho hujawahi kukiona,utaelewa kitu gani?

Pamoja na hayo,maandiko yameeleza vizuri kabisa ni nini kitaanza na kitafuata nini,soma maandiko utaona mwenyewe kati ya jina la mnyama na mnyama mwenyewe ni kipi kilianza....
 
Back
Top Bottom