Naomba ufafanuzi katika hili gari aina ya Toyota Vitz old model Piston 4

Africa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2015
Posts
1,504
Reaction score
2,272
Wakuu
Nimebahatika kupata gari hiyo Vitz old model miezi michache iliyopita, nimeona nije niulize maswali kuhusu hiyo gari mabosi mnaaita "babywoka"

1. Naweza kusafiri nayo from Dar - Mbeya non stop?

2. Vitu gani kiufundi niviepuke kwenye matumizi ya gari hii!?

NB: Engine CC 990, Piston 4

Karibuni!
 
1. Mkuu usijaribu kuichosha kwa hiyo safari labda kama tayari umeichoka.

2. Ngoja waje.
 
Mimi nashauri bora upande basi Masafa marefu ni risk kubwa sana kwa gari ndogo kama iyo
 
Asikutishe mtu mkuu kisa una ki babywoka. Hakuna kitu kuchosha gari, labda ujichoshe wewe dereva. Kama engine yako haina tatizo, macho yako yawe kwenye temperature tu, hiki ndio kitu pekee ambacho kinaweza kukulazimu usimame na gari ipoe ndio uendelee na safari.

Mtu akikwambia sijui engine inachoka ujue ni story za maskani tu hayupo serious.
 
Aisee watanzania tunapenda kutishana Sana!!!
hiyo gari yako inauwezo WA kwenda mbaya bila shida yeyote Ile kitu cha msingi ni kufanya service kuanzia Tu jitahid umpate fundi mwenye kujua Magari atakushauri kilakitu na utafurahi na Safar ndefu
pia zingatia kusafisha rejeta na kutumia coolant ili gari isichemshe njian....

Madereva wa IT kilasiku wanapeleka Magari (kirikuu) Zambia na Malawi sembuse hiyo vitz!!!!
 
Shukrani Mkuu!
 
Asikutishe mtu mkuu kisa una ki babywoka. Hakuna kitu kuchosha gari, labda ujichoshe wewe dereva. Kama engine yako haina tatizo, macho yako yawe kwenye temperature tu, hiki ndio kitu pekee ambacho kinaweza kukulazimu usimame na gari ipoe ndio uendelee na safari.

Mtu akikwambia sijui engine inachoka ujue ni story za maskani tu hayupo serious.
Nakuelewa sana mkuu!
 
Mimi nilikua nacho ki vits cha aina hiyo chenye gear box ya manual! Nilichofanya ni kuweka tu coolant kwenye rejeta badala ya maji ya kawaida.

Aisee hivyo vigari vinatembea vizuri tu na kinaenda kokote na bila shida yoyote ile. Tena kwa wewe wa Dar Mbeya, nyoosha tu mguu mpaka Iringa Mjini, Mafinga au hata Makambako bila kusimama sehemu yoyote. Ukifika hayo maeneo, ndipo usimame na kukapumzisha walau kwa dk 30 mpaka saa 1 hivi huku mwenyewe ukipata chochote na kenyewe kakiwa silence.

Baada ya hapo, unakamua mpaka Mbeya bila hofu yoyote. Vits ni gari ngumu na stable sana barabarani. Huwa hakayumbi ovyo kama akina corolla.
 
Shukrani Mkuu
 
Ukifika hayo maeneo, ndipo usimame na kukapumzisha walau kwa dk 30 mpaka saa 1 hivi huku mwenyewe ukipata chochote na kenyewe kakiwa silence.
gari haipumzishwi kwa silence, unatakiwa uzime mara moja na hasa kama umetembea non stop masafa makubwa. Ni gari yenye turbo tu ndio unatakiwa usubirie kidogo kabla ya kuzima, tena hio ni kwa sababu ya hio turbo sio engine.
 
Unaenda vizuri sana wala wasikutishe, mimi nimetembea na Duet piston tatu toka Dar mpaka Tanga nikageuka mpaka Arusha nilipumzika Tanga kidogo kama nusu saa tuu lakini gari haikuchemka wala kunisumbua na temperature ilikuwa normal na nilikuwa natembea mia ishirini hadi 16o poa tuu
 
Unaweza kwenda nalo bila shida yoyote ile cha msingi zingatia yafuatayo..

1.Engine iwe haina ugonjwa wowote na ufanye service nzuri ya oil na filter

2.Gear box iwe safi na fluid yake iwe kwenye level inayotakiwa na iwe haijachoka..

3.Mfumo wa upoozaji uwe unafanya kazi vizuri ..

Angalizo.....Engine hii ni ndogo, usishindane na wenye brevis huko barabarani....waache waende zao...kwanza huwajui iweje uanze ligi na watu usiowajua..[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]

Uendeshaji wako uwe wa kawaida RPM 2 ikizidi 2.5....

Mwishowe nikutakie safari njema,ukifika Mikumi kuna jamaa yangu atakupatia pembe mbili za Ndovu, kuna mwarabu atazipokea hapo Mbeya..[emoji119][emoji119][emoji119][emoji119]
 
Umeanza vizuri umemaliza na kuniua[emoji3][emoji3][emoji3][emoji706]
 
Back
Top Bottom