Africa Tanzania
JF-Expert Member
- Jun 13, 2015
- 1,504
- 2,272
Fafanua mkuu, nikiichosha kuna loss gani nitaingia?1. Mkuu usijaribu kuichosha kwa hiyo safari labda kama tayari umeichoka.
2. Ngoja waje.
🦾Inaenda fresh tu ila isiwe kila simu
Shukrani Mkuu!Aisee watanzania tunapenda kutishana Sana!!!
hiyo gari yako inauwezo WA kwenda mbaya bila shida yeyote Ile kitu cha msingi ni kufanya service kuanzia Tu jitahid umpate fundi mwenye kujua Magari atakushauri kilakitu na utafurahi na Safar ndefu
pia zingatia kusafisha rejeta na kutumia coolant ili gari isichemshe njian....
Madereva wa IT kilasiku wanapeleka Magari (kirikuu) Zambia na Malawi sembuse hiyo vitz!!!!
Nakuelewa sana mkuu!Asikutishe mtu mkuu kisa una ki babywoka. Hakuna kitu kuchosha gari, labda ujichoshe wewe dereva. Kama engine yako haina tatizo, macho yako yawe kwenye temperature tu, hiki ndio kitu pekee ambacho kinaweza kukulazimu usimame na gari ipoe ndio uendelee na safari.
Mtu akikwambia sijui engine inachoka ujue ni story za maskani tu hayupo serious.
Fafanua mkuuMimi nashauri bora upande basi Masafa marefu ni risk kubwa sana kwa gari ndogo kama iyo
Ni kweli kabisa MkuuKuweza inaweza sana tuu ila isiwe mazoea unajua gari chini ya cc 1000 sio gari za masafa marefu japokuwa zina uwezo huo.
Shukrani MkuuMimi nilikua nacho ki vits cha aina hiyo chenye gear box ya manual! Nilichofanya ni kuweka tu coolant kwenye rejeta badala ya maji ya kawaida.
Aisee hivyo vigari vinatembea vizuri tu na kinaenda kokote na bila shida yoyote ile. Tena kwa wewe wa Dar Mbeya, nyoosha tu mguu mpaka Iringa Mjini, Mafinga au hata Makambako bila kusimama sehemu yoyote. Ukifika hayo maeneo, ndipo usimame na kukapumzisha walau kwa dk 30 mpaka saa 1 hivi huku mwenyewe ukipata chochote na kenyewe kakiwa silence.
Baada ya hapo, unakamua mpaka Mbeya bila hofu yoyote. Vits ni gari ngumu na stable sana barabarani. Huwa hakayumbi ovyo kama akina corolla.
gari haipumzishwi kwa silence, unatakiwa uzime mara moja na hasa kama umetembea non stop masafa makubwa. Ni gari yenye turbo tu ndio unatakiwa usubirie kidogo kabla ya kuzima, tena hio ni kwa sababu ya hio turbo sio engine.Ukifika hayo maeneo, ndipo usimame na kukapumzisha walau kwa dk 30 mpaka saa 1 hivi huku mwenyewe ukipata chochote na kenyewe kakiwa silence.
Umeanza vizuri umemaliza na kuniua[emoji3][emoji3][emoji3][emoji706]Unaweza kwenda nalo bila shida yoyote ile cha msingi zingatia yafuatayo..
1.Engine iwe haina ugonjwa wowote na ufanye service nzuri ya oil na filter
2.Gear box iwe safi na fluid yake iwe kwenye level inayotakiwa na iwe haijachoka..
3.Mfumo wa upoozaji uwe unafanya kazi vizuri ..
Angalizo.....Engine hii ni ndogo, usishindane na wenye brevis huko barabarani....waache waende zao...kwanza huwajui iweje uanze ligi na watu usiowajua..[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]
Uendeshaji wako uwe wa kawaida RPM 2 ikizidi 2.5....
Mwishowe nikutakie safari njema,ukifika Mikumi kuna jamaa yangu atakupatia pembe mbili za Ndovu, kuna mwarabu atazipokea hapo Mbeya..[emoji119][emoji119][emoji119][emoji119]
Shukrani MkuuUnaenda vizuri sana wala wasikutishe, mimi nimetembea na Duet piston tatu toka Dar mpaka Tanga nikageuka mpaka Arusha nilipumzika Tanga kidogo kama nusu saa tuu lakini gari haikuchemka wala kunisumbua na temperature ilikuwa normal na nilikuwa natembea mia ishirini hadi 16o poa tuu